4.2
4.2
Katika toleo hili, utajifunza jinsi Mungu anavyofanya kazi huko Afrika Kaskazini akitumia biashara na elimu kuwaunganisha wenyeji kupitia mkakati wa “Nenda Kaskazini”. Utasoma simulizi za kushangaza kuhusu uaminifu wa Mungu katika maisha ya Mchungaji Johnson Asare, msomi, mmishonari na mfanyabiashara, na katika maisha ya Bwana Septi Bukula, kiongozi wa umisheni na mfanyabiashara. Utafahamu jinsi hadithi ya Msamaria Mwema, kama ilivyotumiwa na Mchungaji Asare ilivyosaidia ufahamu wake wa kibiashara na kazi ya umisheni. Ndugu Bukula anashirikisha ufahamu wake juu ya masomo aliyojifunza kutoka kwa baba yake kuhusu kufanya kwa pamoja biashara na umisheni, ukilinganisha na yale mahubiri yaliyokuwa yanaenezwa na makanisa yakikatisha tamaa kwa kudai kuwa Wakrsito wanatakiwa kupokea baraka lakini hawahusiki kutumia utajiri wao kwa ajili ya watu wengine.
Wajibu Wa Biashara Katika Umisheni
Kuna hadithi moja inayohusu kundi la watu walioishi karibu na pwani. Baada ya miaka kadhaa wakishuhudia ajali za kuzama kwa meli baharini na matokeo yake ni kupotea kwa maisha ya watu na mali, waliamua kufanya jambo fulani kuhusu hali hiyo. W...
Mungu Hakutengeneza Meza; Aliumba Miti
Kuna uhusiano gani kati ya hadithi ya Msamaria Mwema na Biashara ya Kimisheni? Au biashara yo yote kwa ujumla? Johnson Asare, mwanzilishi na Mkurugenzi wa kitaifa wa huduma za Markaz Al Biashara huko Tamale, Ghana, anatoa funzo la kutufungua ...
Mercy Kambura
‘Njoo Huku Utusaidie’
Ni nani bora zaidi kuwafikia Waislamu wa Afrika isipokuwa Wakristo wa maeneo mengine ya Afrika? Hayo ndiyo yaliyokuwa mawazo ya mwaka wa 2011 wakati wa Mkutano wa Vuguvugu la Mkakati wa Mataifa ya Afrika (MANI), ambalo lilizalisha kwa mkakati...
Walioitwa: Septi Bukula – Kusudi la Biashara ni nini?
Nilipoulizwa swali hili yapata miaka 14 iliyopita, nilifikiri nilijua Jibu lake. Wakati huo nilikuwa nahudhuria kongamano huko Jakarta nchini Indonesia, pamoja na waumini kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Baada ya juma moja la majadiliano...
Makundi ya Watu: Gujarati
Wagujarati ni kundi la watu ambalo limetawanyika sana takriban katika mataifa 129 na wanajumuisha asilimia 33 ya Wahindi wote walioko ughaibuni kote duniani. Asili ya Wagujarati ni katika jimbo la Gujarat Magharibi mwa India, na lugha yao ni ...