Skip to content

Kumwezesha mshirika wako kuingia katika umisheni

Mchungaji Faith Mugera

Nairobi Chapel ni kanisa kubwa lenye nia ya umisheni nchini Kenya. Wametuma wamishenari 31 na timu 33 za muda mfupi na wana matokeo katika nchi 16. Faith Mugera, mchungaji wa umisheni, anashirikisha mawazo sita ambayo wameanzisha ili kuratibu programu yao ya umisheni.

1. Thibitisha wito wao Jua safari iliyopelekea uamuzi wao. Washirika wetu hawaendi peke yao, kwa hivyo tunataka kuelewa jinsi tunavyoweza kuthibitisha na kuhusika na wito wao.

2.Ujenzi wa tabia

Tunawasilisha mafunzo ya uanafunzi na tunasihi ili kuwatayarisha na kuwategemeza katika wakati wao wakiwa mbali. Ni muhimu kwamba hii iendelee kwenye eneo watakaloenda.

3. Mafunzo ya utamaduni

Kuanzia na mawazo ya kimsingi kuhusu utamaduni, tunataka wazamishwe, wavunje fikra potofu, wasikilize vyema, wawe sehemu na wajenge mahusiano yanayodumu.

4. Kujidhatiti/Kujitoa kwa dhati kwa ajili ya wito

Tunawaomba washiriki wetu waweke viapo vya utauwa, usafi, na umaskini, au karibu na hizi kama ilivyokubaliwa.

5. Kuwaagiza

Tunamsherehekea na kumtuma mmishenari hadharani. Kwa kawaida tunafunza vikundi vyao vidogo kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwatembelea, kupiga simu, na kutuma vifurushi vya zawadi.

6. Kanisa

Daima tunashirikiana na kanisa la nyumbani. Wanashughulikia visa, bima, na malazi. Tunawategemeza wamishenari wetu kifedha, kwa hiyo hawajahitaji kutafuta ufadhili.

Faith Mugera, Mchungaji wa Ushirikiano wa Kimataifa na Umisheni, Nairobi Chapel.

Other articles and resources from around the web on this topic: