Skip to content
AfriTWENDE logo

Mungu ametuita kwenda kwenye ulimwengu kuwaambia watu kuhusu yeye. Waafrika wamekua wakifanya hivi kwa karne nyingi, lakini habari zao nyingi hazijawahi kusemwa. AfriTWENDE inatuambia habari za wamisionari wa kiafrika na kusambaza taarifa zao mpya kwenye harakati za umisheni Afrika.

Soma jarida letu la kila robo mwaka ili uweze kuhabarishwa mada mbalimbali kuhusu umisheni.

Fatilia mitandao yetu ya kijamii ili uweze kutiwa moyo mara kwa mara.

 

Soma habari za wamisioanari kwenye lugha ya kiswahili na sambaza kwa watu wengine.

 

Tembelea rasilimali zetu za bure juu ya uislamu uweze jifunza ni kwa namna gani unaweza kuwafikia majirani zako.

Masuala yaliyopita

Boti iliyo mbali ni simulizi ya kubuni ya Max, kijana Mkenya wa mjini, ambaye alikuwa na vyote: kazi ya ndoto zake, rafiki wa karibu, na msichana anayetarajia kumwoa. Akiwa katikati ya shida, Max alikutana na kitu cha ajabu, pale alipokutana na mvuvi mmoja masikini aliyekuwa Mwislamu, jina lake ni Yusuf. Maisha yote na mtazamo mzima wa Max ulitatizwa na kutiwa changamoto alipotambua Kuwa Yusuf na watu wake hawana na kanisa na hakuna hata shahidi wa mkristo wa kuwashuhudia. Baada ya kupata muda wa kupumzika, alimtembelea mjomba mzee mwenye hekima na alimshirikisha jinsi alivyoguswa na habari za Yusuf na watu wake, na katika mchakato huu, Max alitambua kuwa Mungu alikuwa akimwita ili awe mmisionari.