“Jehanamu ni halisi” – hadithi za kimishenari
Jina langu ni Mustafa Abubakar.Tulilelewa kwenye familia yenye itikadi kali ya Kiislamu, tukahudhuria Madrassa na kupata mafundisho yote ya Kiislamu.
Roho yangu haikupata amani kamwe. Nilijua bila shaka kuwa jehanamu ni halisi, kwani Uislamu ulinifundisha hivyo. Katika Uislamu, wokovu unategemea matendo mema; watu huamini kuwa matendo hayo ndio yatawapeleka mbinguni. Mimi mwenyewe nilihisi wazi kuwa nilikuwa nikielekea moja kwa moja motoni.
Nilikuwa na maisha ya uzinzi. Nilikuwa mraibu wa ngono na pia nilizama kabisa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Hatimaye, niliacha chuo kikuu kwa sababu ya hali hiyo. Nilihisi kukata tamaa kabisa. Mara nyingi ningeenda Uhuru Park, nikatazama angani na kulia kwa huzuni kuu. Moyoni nilihisi shimo kubwa la maumivu.
Furaha na amani ziliniikwepa kila mara. Nilijaribu kwa nguvu zangu zote kufanya mema, lakini nilizidi kushindwa. Nilijua siwezi kuwa mzuri vya kutosha, na hilo liliniletea hasira.
Nilitamani kupata uhakika wa kwenda mbinguni, jambo ambalo Uislamu haukunipa. Ilibainika wazi kuwa kama nitategemea matendo yangu mema, basi mimi nitaangamia kabisa.
Mwishowe, nilisikia injili ikihubiriwa kutoka katika Waebrania 9:27. Mhubiri alizungumzia dhambi za mwanadamu, utakatifu wa Mungu, na hukumu inayokuja.
Nilirudi nyumbani baada ya mkutano, nikachukua Biblia na kuisoma kutoka Mwanzo hadi Ufunuo kwa muda wa miezi mitano.
Na safari ilianza… hadi leo. (Sasa) Ninahudumu pamoja na ndugu wawili, tunafanya upandaji wa kanisa huko Mombasa.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza https://afrigo.org/story_resources/missionary-profile-mustafa-abubakar/