Mpango Wa Umisheni Wa Malawi Unakuza Uinjilisti Wa Kuvuka Mpaka
Makongamano ya kikanda ya wachungaji wenye wito wa kimisheni yaliandaliwa na SIM kwa ushirikiano na Chama cha Kiinjili cha Malawi. Makongamano hayo huchochea hamasa miongoni mwa makanisa ya Malawi kuvuka mpaka kwa ajili ya kuwafikia wengine. Matokeo yake yalikuwa ni kuanzishwa kwa mpango unaojulikana kama Mpango wa Umisheni nchini Malawi (Malawi Mission Intiative-MMI), ulioanzishwa mwaka 2013 na Ushirika wa Kiinjili wa Malawi (the Evangelical Association of Malawi-EAM) kwa ushirikiano na SIM
MMI ni mtandao wa Makanisa yanayojali umisheni na wakala wa umisheni ili-kuwezesha uhamasishaji na kutoa msaada wa kazi ya umisheni wa kuvuka mipaka. Mchungaji Paul M.L. Mawaya wa SIM, ambaye ni mhamasishaji wa kitaifa nchini Malawi, anaendeleza kazi ya MMI kupitia Ukuzaji wa Ushirika wa Maombi wa Malawi. Vikundi hivi vya kuomba pamoja vinashiriki katika kupanga mafunzo, shughuli za uinjilisti, maombi na kuhamasisha makanisa kufanya umisheni kwa Waislamu. Pia husaidia wamishenari ambao wanahudumu katika maeneo ya umisheni na kuandaa makongamano ya kutia moyo watu kujitokeza na kuvuka mipaka ya kiutamaduni kwa ajili ya kazi za umisheni.
Mpaka sasa, Mchungaji Gusty na mkewe Ellina Makhutcha wametumwa kwenda kuhudumu kama wamishenari miongoni mwa kabila la Wayao ambao wanaishi nchini Msumbiji. Mchungaji Gusty anasaidiwa na Kanisa la Kibaptisti la Blantyre nchini Malawi. Katika ushirikiano huo huo Ndugu Francis Kuntenga ameanza kufanya kazi na kabila la Wayao huko nchini Malawi upande wa mpakani na Msumbiji.