fbpx Skip to content

Mashua iliyo Mbali

‘Mashua iliyo mbali’ ni filamu ambayo inalialika kanisa la Kiafrika katika kushikilia fursa ya kipekee ya kuwafikia Waafrika ambao bado hawajafikiwa na Injili; kwa kutoa changamoto kwa kanisa ya kuwa na nguvu kuu kwa ajili ya umisheni huko mbeleni.

Ni habari ya Max, kijana Mkenya anayeishi mijini. Max ana ndoto ya kupata kazi nzuri, rafiki na mchumba ambaye atamuoa baadaye. Baadaye Max anakutana na Yusuf, mvuvi na mwiislamu. Yusuf na watu wake hawana kanisa wala mkristo wa kuwashuhudia. Hali hii inamsukuma Max afikirie kama Mungu anamwita ili awe mmishenari.

Filamu hii ya dakika 120 ilitayarishwa na taasisi ya On Field Media (Huduma ya misheni ya AIM) kwa ushirikiano na washirika wengine. Inaonyesha gharama, vikwazo na namna ya kuvishinda kama kanisa linataka kuyafanya mataifa yote kuwa wanafunzi. Unaweza kuiangalia filamu hii kwenye https://distantboat.com/swahili/

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us