Skip to content

Coming soon!  Our latest issue on Training.  Do you need it?  What do you need?  Watch this space!

AfriTwende

Kulitia moyo
Kanisa katika
ulimwengu wa umisheni

Kwa zaidi ya karne, waafrika wamejitoa kutumikia katika utume, kuwarudisha waliopotea kwa Yesu Kristo na kusimika makanisa. Lakini karne mbili zilizopita zilikuwa kama karne za mazoezi au kupasha moto tu katika bara la Afrika, ambapo sasa kanisa limeimarika vizuri na Roho Mtakatifu akiendelea kuwaita watenda kazi katika utume kwenye jamii yenye mwingiliano wa tamaduni.

Ili kuchochea moto wa harakati za kitume, AfriGO ilianzishwa mwaka wa 2016. Jarida hili la AfriGO linalotolewa kila baada ya robo mwaka linasherehekea historia hiyo huku ikilitia moyo kanisa kuongeza ushiriki wake katika mpango wa kitume wa Mungu duniani. Wakati Kanisa la Afrika likitoa uongozi mpya na watenda kazi kuitangaza injili, AfriGO ipo kuwasimulia, kuwapa taarifa juu ya maendeleo hayo, na kuwashirikisha taarifa ili kuwaunga mkono wachungaji na wafanyakazi waliowatuma.

Ombi letu ni kwamba sauti za waafrika zinazozungumza kupitia chapisho hili zitachochea kupeleka mbele harakati mpaka upendo na utukufu wake Mungu utakapotangazwa duniani kote.

Past Issues

Jisajili