Skip to content

Nenda kwa kasi zaidi ya upepo kama ilivyosimuliwa

Mercy Kambura

Hebu fikiria kundi la vijana motomoto katika safari ya umisheni kwenda kwenye kundi la watu ambao ha wajafikiwa kusini mwa Angola. Wana kaa kwa mwezi mmoja, wakihubiri, wakivunja vifungo, na kuwapatanisha wanakijiji na Muumba wao. Hatimaye, ni wakati wa kwenda nyumbani, lakini mavuno bado ni mengi. Mmishenari an gefanya nini?

Nilikumbana na hali hii miaka mingi iliyopita. Kijana mmoja aliamua kwamba hatakuwa akifuatana nasi wakati wa kurudi nyumbani baada ya umisheni wa muda mfupi. Nilikuwa kiongozi wake, mwenye jukumu la kumrudisha yeye na wengine 14 kwa wazazi wao. Nikiwa na wasiwasi, niliripoti uamuzi wake kwa mama yake, nikitarajia kuadhibiwa. Lakini alisema, “Siwezi kupigana na Mungu. Ikiwa anataka kuwa mmishenari, na iwe hivyo.”

Nikiwa kijana, tulicheza mechi na marafiki zetu. Siku moja, mtu fulani alipendekeza kwamba tusali mwisho wa mechi. Tulifurahia kusali pamoja sana mpaka ikawa tabia. Kila Jumapili, baada ya mchezo, tungekusanyika ili kuomba. Hivyo ndivyo nilivyookolewa.

Kikundi kidogo cha maombi kikawa kikundi cha kujifunza Biblia, na tulikuwa tukikutana mara tatu kwa juma. Miaka mitatu baadaye, kikundi hicho kikawa kanisa. Tulikua na washirika zaidi ya 100. Sote tulikuwa vijana bila uzoefu mwingi; kwa hivyo, tulimwalika kaka mmoja mwenye umri mkubwa kuliko sisi atuongoze na kuwa mchungaji wetu.

Kanisa hilo sasa lina umri wa miaka 15 na waumini zaidi ya 2000, wengi wao wakiwa vijana. Furaha yetu kuu sio idadi yetu, lakini kuhusika kwetu katika Agizo Kuu. Maneno ya kanisa letu, Born Again Church (Igreja Nascidos de Novo) huko Luanda, Angola, ni “huduma inayoleta matokeo katika mataifa.”

Kila juma, tunahubiri mtaani. Kama wachungaji, tunaenda nao. Tunalifundisha kanisa kufanya uinjilisti kuwa mtindo wa maisha. Kila mtu anapaswa kuhubiri na kuwafanya watu watano hadi saba kuwa wanafunzi. Tulipanga ratiba na kueneza injili katika hospitali 16 tofauti.

Sasa ninatumika kama makamu wa rais wa kanisa. Mungu aliniita kuwa mmishenari baada ya safari yangu ya kwanza ya umisheni wa muda mfupi. Tunataka kanisa letu lihusike katika umisheni hadi uwe utamaduni wake. Makanisa mengi hayashiriki katika umisheni kwa sababu waumini hawajui jinsi ya kukutana na watu wapya na kuwashirikisha Injili.

Kukuza kanisa la kimisheni

Uinjilisti sio kazi ya wikendi au likizo tu. Ni lazima ifanyike kila siku.

Kanisa barani Afrika linapaswa kwenda kwa kasi zaidi kuliko upepo ili kueneza Injili kwa waliofikiwa kwa uchache. Je, Kanisa linawezaje kufikia hili?

  1. Usipoteze nafasi yoyote ya kuhubiri kila mahali.
  2. Tumia nguvu, wakati, na shauku ya vijana na ufanye nao kazi.
  3. Endesha mafunzo ya kila wiki ya jinsi ya kushirikisha Injili.
  4. Kumbuka kwamba kiini cha Ukristo ni umisheni. Yesu hakutuambia tukumbuke zaka na kadhalika. Akasema, “NENDA!” Mpendwa Mchungaji, usiruhusu kitu kingine chochote kuchukua nafasi ya maana ya Kanisa. Utume wa Kanisa ni kwenda. Ikiwa hutamwokoa jirani yako, je, unaelewa kweli kwa nini umeokolewa?

TAFADHALI OMBA:

  • Kwa ajili ya rasilimali na fedha wakati tunaposafiri.
  • Kwa ajili ya magari mazuri kwa ajili ya kwenda sehemu ngumu.
  • Kwa ajili ya watenda kazi zaidi katika shamba la umisheni. Mavuno ni mengi.
Other articles and resources from around the web on this topic: