Makundi la Watu: Wabeja wa Eritrea, Sudan, na Misri
Kabila la Wabeja ni kundi la watu wanaohamahama ambao wamekuwa wakiishi katika nchi za Sudan, Eritrea, na Misri kwa zaidi ya miaka 4,000. Katika historia yao, waliukubali Uislamu na asilimia 99 ni Waislamu. Wanatekeleza Uislamu wa mchanganyiko na dini za asili na wanaamini katika jicho baya na majini. Wanajaribu kupata nguvu kutoka kwao kwa kutumia hirizi.
Wabeja ni kundi la watu ambao huonekana kama sio wa muhimu na ni maskini. Wakiwa ni idadi ya takribani watu milioni 4, wengi wao wana elimu ndogo au hawana kabisa na wanachukuliwa kuwa watu wa tabaka la chini na wananchi wenzao. Mazingira yao ya kuhamahama yanapungua na wengi wanahamia mijini kutafuta kazi za mikono na zenye malipo duni. Mtu asiyekuwa Mbeja atapendelewa kila wakati kuliko Mbeja wakati wa kuajiri.
Sababu moja ya kwa nini hawajafikiwa kabisa ni kwamba ili kuwafikia, mmishenari atalazimika kuishi katika mazingira magumu mbali na maeneo ya mijini. Huko nchini Sudan, Misri, na Eritrea, Wakristo wametambua kwamba Wabeja wanamhitaji Yesu, na wameanza kusikia msukumo wa kuwafikia. Kijana mmoja amehamia mahali pa mbali ili kuwafikishia injili. Wengine katika miji wameanza kutoa maji baridi au juisi kwa watu wa kundi la Wabeja ambao hupita karibu na kanisa lao. Wengine wameanza kupeleka chakula kwa wafungwa wa kabila au kundi la Wabeja.
Wabeja wanazidi kukatishwa tamaa na serikali za Kiislamu zinazojaribu kufuta utamaduni na lugha yao. Katika maeneo fulani, wanaomba shule za Kikristo kwa watoto wao na kuomba wamishenari. Walakini, idadi inayoufuata Ukristo bado ni ndogo sana.
KWA KIFUPI
- Abu Nasr Mutahhar al-Maqdisi, aliandika katika karne ya kumi kwamba Wabeja walikuwa Wakristo wakati huo.
- Wabeja hufunga ndoa kati ya mtu na binamu yake.
- Baadhi ya Sehemu tu za Maandiko ziko katika lugha yao ya Bedawiyet
OMBA KWA AJILI YA
- Maandiko zaidi na nyenzo zitafsiriwe kwenda lugha yao ya Bedawiyet.
- Wakristo wenyeji wasikie msukumo wa Roho Mtakatifu na kuwafikia Wabeja.
- Wabeja wamjue Yesu na kuanza harakati miongoni mwa watu wao.
Vyanzo: http://bejafriends.org/ • https://joshuaproject.net/people_groups/10766 • https://omniglot.com/writing/beja.htm https://en.wikipedia.org/wiki/Beja_people