Skip to content

Mambo yawa Mazuri kwa Reagan

Kate Azumah

Regani alikuwa hajawahi kutoka nje ya mji wa Kumasi. Siku ambayo Reagan alipanda basi kutoka Kumasi kuelekea eneo la umisheni mbali na nyumbani kwao ilikuwa siku ya kipekee. Alipofika Tamale, aligundua kwamba basi la kwenda Gbintre lilisafiri mara moja tu kwa siku. Hakulikosa, lakini alitamani angalau angekuwa amelikosa. Kwanza, basi lilitikisika vibaya sana! Kisha mvua ikanyesha, na licha ya kuwa ndani ya basi, lakini alilowana mwili mzima.

Muda uliokuwa umepangwa kufika ilikuwa ni saa 3 usku badala yake wakafika saa 6 za usiku wa manane. Alilala huko Gbintre na kuendelea na safari siku iliyofuata. Alikuwa akitarajia gari zuri ambalo lingemsafirisha yeye na mwenzake, Joseph, hadi kule wanakokwenda. Badala yake, walipanda kwenye baiskeli ya miguu mitatu isiyo na paa pamoja na wanawake wa sokoni ambao walizungumza lugha ngeni. Reagan anasimulia, “Hatimaye tulipofika Tuna, kijiji hicho hakikuwa na umeme. Usiku, giza lilikuwa nene sana sikuweza kuona nyuso za watu. Mama yangu alikuwa sahihi. Hapa ni mahali pa mateso, na sikupaswa kuja kamwe.”

Wito wa Reagan

Reagan Opoku Agyeman alihitimu shahada ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah huko Kumasi, Ghana. Uamuzi wake wa kujisajiri kuwa mmishenari wa shirika la Operation Serve ulitokana na ushawishi wa rafiki yake, Razak. “Nilipokuwa nikimaliza shule, Razak aliniambia kuhusu fursa ya kufanya kazi ya umisheni wakati nikiwa Kwenye Mpango wa Huduma ya Kitaifa. Niliamua kuliombea jambo hilo. Sikuona maono yoyote au kusikia Bwana akizungumza, lakini niliamua kwenda kwa utii rahisi.”

Wasiwasi wa familia

“Nilijua ningewaambia wazazi wangu naenda kufanya umisheni, jibu lao lingekuwa ‘hapana’ moja kwa moja. Kwa hiyo, nilipanda wazo akilini mwao kwamba kwa kuwa nilikuwa nimebobea katika Usimamizi wa Kilimo Biashara, kutumika Kaskazini kungekuwa faida ya kitaaluma. Mama yangu alisema atakuwa radhi na hilo.”

Utumaji ukafika na Reagan alitumwa katika kijiji cha mbali cha Tuna katika wilaya ya Bunkpurugu katika mkoa wa kaskazini Mashariki. “Mama alikasirika; Baba, binamu, shangazi, na bibi walipinga. Dada mdogo wa Mama yangu aligombana na mimi na kusema hataniruhusu niende. Rafiki mmoja aliniuliza kwa nini nilikuwa mpumbavu hivyo. Uhasama ulikuwa dhahiri. Niliwaambia ni kwa mwaka mmoja tu, lakini hawakuridhika.”

Mama alikasirika; Baba, binamu, shangazi, na bibi walipinga.

“Kwa mara ya kwanza maishani mwangu, niliamua kusimama mwenyewe. Niliwaambia nina umri wa kutosha kufanya maamuzi yangu mwenyewe.” Reagan aliondoka nyumbani kwa muda wa wiki sita za mafunzo ya umisheni. Familia yake haikumzuia, lakini shida zake hazikuisha. “Nilipokuwa shule ya umisheni, Baba alinipigia simu alfajiri moja, na kuniomba nirudi nyumbani. Alikuwa akiongea kwa hisia sana.”

Mama wa Reagan, Mama Anna, anaeleza, “Hakuna hata mmoja wetu aliyefurahishwa na habari hizo. Kaskazini kulikuwa na hali tete, na tulihofia usalama wake.” Baba yake Reagan pia alitarajia mzaliwa wake wa kwanza angepata kazi nzuri na ili kuisaidia familia kifedha.

Maisha ya umishenari Reagan alifundisha katika shule ya msingi ya Tuna, aliendesha huduma kwa watoto, aliratibu ibada za kanisa katika jamii nyingine, na kupitia huduma ya michezo, aliwafuasa wavulana wengi ambao mwanzoni ilikuwa vigumu kuwafikia.

Siku moja, Reagan na Joseph walikuwa wakivumilia joto kali nyumbani wakati Eliya alipoingia ndani kwa ghafla. Mkewe alikuwa akisumbuliwa na homa kali. Walienda pamoja naye na kumwombea. Walipokuwa wakiomba, nguvu za Mungu zilimshika na akaanza kutokwa na jasho. “Mbele ya macho yetu, aliponywa papo hapo! Sikuwa mtu wa kiroho sana, kwa hiyo nilishtuka. Iliniingia moyoni kwamba Mungu hakunileta hapa kwa ajili ya kujifurahisha, bali kwa ajili ya umisheni wa kweli.” Huu ulikuwa mwanzo wa shuhuda nyingi huku watu wengi wakimiminika kuja kwa ajili ya maombezi.

Walimuombea Sala ambaye alitaka kupata mtoto. Alipojifungua, aliwaomba wampatie jina. “Tulimwita Muujiza,” Reagan anasema. “Mwanamke mwingine aliye na kifafa alikuja kutoka Kusini kutafuta matibabu kwa mganga wa kienyeji huku Kaskazini. Tulimwomba aje kijijini kwetu kwa ajili ya maombezi. Siku iliyopangwa, kijiji chake chote kilikuja pamoja naye. Walitaka tuwaombee pia. Yule Mwanamke sasa ni mzima kabisa.”

Wakati alipokuwa nyumbani kutoka eneo la umisheni, Reagan alishirikisha shuhuda hizi kwa familia yake. Walianza kuacha kumsumbua, lakini walimkumbusha ahadi yake kwamba ilikuwa ya mwaka mmoja tu.

Wanaona kwamba kitu kizuri kimetokea ndani yake.

Reagan alipitia nyakati ngumu pia. Katika siku yake ya kwanza akiwa kwenye eneo la umisheni, alikuwa mgonjwa sana. Alipompigia simu mama yake akasema, “Njoo nyumbani. Tutakuhudumia.” Reagan alibaki hakuenda. Kuwasiliana kwa simu kulikuwa kunakatisha tamaa. “Mahali pekee ningeweza kupata mtandao ilikuwa karibu na mti fulani. Ukitembea kidogo tu na mtandao unapotea.” Mama Anna analalamikia hili kuwa ni wasiwasi mwingine kwa familia. “Hatukuweza kumpigia simu kwa wakati wowote tulipotaka. Ilibidi tumsubiri yeye ndo atupigie.”

Msaada kwa familia

Ingawa alipata kipato kidogo, Reagan alituma pesa kwa wazazi wake na ndugu zake mara kwa mara. Walifurahishwa na jitihada zake. Baada ya kutumika mwaka mmoja na shirika la Operation Serve, alijiunga na shirika la OneWay Africa kama mmishenari wa wakati wote. Kwa sasa yuko katika mwaka wake wa nne, na anasafiri kwa pikipiki yake akionyesha Filamu ya Yesu miongoni mwa jamii za Wagonja zilizofikiwa kwa uchache kaskazini mwa Ghana.

Familia ya Reagan sasa inaomba kwa ajili yake na kusaidia huduma yake kifedha. Wanaona kwamba kitu kizuri kimetokea ndani yake.

Wazazi wa Reagan

Mawazo ya mama

Wasiwasi wa usalama wa Reagan haukumpa Mama Anna utulivu. Siku hizi, anasema, “Baadaye, nilitafakari na kuomba. Niligundua Mungu ndiye anayemlinda na sio sisi. “Tunafurahi kwamba anapata kipato cha kutosha kujikimu. Kuna wahitimu wengi wasio na kazi ambao bado wanategemea wazazi wao. Umisheni ni kazi nzuri, kwa hiyo tunamuunga mkono.”

Mama Anna aliharibikiwa mimba nane kabla ya Reagan. Anatambua mkono wa Mungu juu yake, na hapingi. Huwashauri wazazi akisema: “Kumwachilia mtoto ayaendee yasiyojulikana si rahisi, lakini huna uwezo wa kumlinda. Wangeweza kuchagua njia ambayo ingekuletea matatizo na maumivu ya moyo. Wakichagua umisheni, waombee na uwaunge mkono.”

OMBA KWA AJILI YA

  • Jamii za Wagonja zilizofikiwa kwa uchacheilli wamjue Kristo.
  • Reagan na wamishenari wote wanaowafikia Wagonja ili Mungu awalinde.
  • Neema ya pekee ya Mungu na amani kwa wazazi wa wamishenari wanaohudumu katika maeneo ya mbali.