Skip to content

Nimeitwa: Ralambo Tiffanie Siko Mpweke Tena

Kama ilivyosimuliwa kwa Mercy Kambura

Nilitiliwa shaka nilipowasili kwa mara ya kwanza kama mmishenari hapo Kisiwani. Sikujua kwamba baadhi ya wanawake wa Kimalagasi ambao waliofika kabla yangu. Ilikuwa vigumu kuishi nikiwa msichana mmishenari wa Kimalagasi ambaye hajaolewa. Nilipata shida sanakupata marafiki, lakini ilinibdi nikae tu kwa ajili ya Injili. Kama mzaliwa wa katikati katika familia ya watoto saba, nilikuwa mtoto wa bango la kujihurumia. Kuambiwa maneno mazuri (ya uthibitisho) na kuwa na wakati mzuri ni jinsi ya kuonyesha upendo, na nilikuwa sipati dozi zake. Familia yangu ilikuwa na uhusiano wa karibu nami, lakini akili yangu changa ilihisi kwamba nilikuwa miongoni mwa walio wadogo zaidi katika familia yangu. Licha ya jitihada zao za kunipa upendo, bado nilihisi hautoshi. Hata hivyo, kunijali kwao kulinifanya niendelee nilipojitolea kuwa mmishenari. Licha ya kuwa msichana ambaye sijaolewa, familia yangu ilikuwa na uhakika kwamba Bwana alikuwa amenituma.

Nilimwamini Bwana wakati nikiwa chuo kikuu. Nilihudhuria ushirika wa ushirika wa Biblia wa Chuo Kikuu (yaani University Bible Group kwa kifupi UBG), na mafunzo ya Biblia yalinivutia. Sikuwa nimewahi kusikia Neno la Mungu kwa uwazi namna hiyo. Licha ya kukulia katika nyumba ya Kikristo, sikuwa bado mtoto wa Mungu, kwa hiyo nilitoa maisha yangu kwa Yesu.

Bwana alinifanya upya na kunipa furaha; sikuwa na hasira tena na familia yangu. Nilipoanza kuzaa matunda, walishangaa kwamba nilikuwa nikipendezwa na mambo ya Kristo. Nilisikia kuhusu umisheni kupitia Usharika wla Biblia wa Chuo Kikuu (UBG). Nilishuhudia jinsi vijana walivyokuwa wanawaka moto kwa ajili ya Mungu. Nikasema, “Yesu, nitakapokua katika imani yangu, nitaenda pia mahali fulani Madagascar kuhubiri Habari zako Njema.”

Nilianza kushiriki katika umisheni na kujifunza kuhusu maisha ya umishenari. Baadaye nilienda kama mmishenari chini ya shirika la kimishenari la AIM hadi visiwa vya Madagascar ili kutumika miongoni mwa watu ambao hawajafikiwa.

Eneo la umisheni lilikuwa na mambo mengi ya kushtua yaliyokuwa yakiningoja. Sikuwa na muda wa kujiandaa. Nilijifunza kila kitu nikiwa tayari shambani, hata vitu ambavyo ningepaswa kujua kwa nadharia. Nilikuwa Mmalagasi pekee kwenye timu yangu, na upweke ulianza kutanda. Wakati fulani, nilitaka kukimbilia nyumbani na kulia. Nilipakumbuka nyumbani, na pia sikuwa na ufadhili wa kutosha wa kifedha. Baada ya mwaka mmoja, nilirudi nyumbani kwenye sherehe kama ya mwana mpotevu kutoka kwa familia yangu.

Kurudi nyumbani, nilianza kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali linalosaidia wanawake. Tuna mradi unaolenga kuhubiri Injili kwa Wahindi hapa Madagascar. Nimekuwa nikimfundisha mwanamke wa Kihindi mwenye asili ya Kiislamu ambaye ndiye mwamini peke yake katika familia yao. Nimeuelewa moyo wa Mungu kwa ajili ya mataifa na sasa ninaona zaidi ya upendeleo wa kitamaduni.

Maisha yangu ni kwa ajili ya Bwana, na ninachagua kuyatumia kwa kitu ambacho kitadumu milele.

Bwana akikuita, nenda. Usisubiri. Sijisikii mpweke tena. Bwana aliniweka katika familia yake ya mbinguni, na uhusiano wangu na familia yangu ya hapa duniani umekuwa bora kuliko ulivokuwa hapo awali. Dada zangu wanatamani zaidi kuwa na uhusiano na Yesu. Familia yangu inaniunga mkono na haijawahi kupinga umisheni ambao nimeufanya.

OMBA KWA AJILI YA:

  • Hatua zangu zinazofuata; moyo wangu unatamani kurudi kwenye huduma ya umisheni. Omba kwamba Bwana aniongoze katika kila nilifanyalo.
  • Familia yangu na mimi tukue katika upendo wetu kwa Yesu Kristo.
  • Jamaa zangu ili wamjue Bwana.