Skip to content

“Mara nyingi, alisimama mlangoni” – nyakati za wamishenari

Happiness alikuja kwetu baada ya wazazi wake waliokuwa wamishenari kuuawa kaskazini mwa Nigeria na watu wenye msimamo mkali wa kidini. Alikuwa na umri wa miaka miwili tu, nami nilimpa jina la Happiness, kinabii nikiamini maneno ya Isaya 51.
Mwanzoni, alikuwa amechanganyikiwa sana na aliweza kulala mchana tu lakini usiku kwake alikuwa amezoea kulinda mlango na kuangalia nje, akiwaza pengine wavamizi walikuwa wanarudi tena. Ingawa alikuwa mdogo sana, alikuwa tayari amepata kiwewe (trauma) kadiri alivyokuwa akipambana na uhalisia wa mazingira yake mapya na uwezekano wa familia yake mpya kuwa kama ndoto iliyoyeyuka.
Walakini, kwa muendelezo mzuri wa kumjali na kumpatia taswira mbadala, kwa vitu kama vile katuni za kibiblia na baadaye kumpeleka shuleni, alipazoea kwa upesi nyumbani kwetu ambapo watoto waliopitia shida huwa wanakaa, na alianza kula na kunywa vizuri, alilala na kucheza kama kawaida ya mtoto yeyote wa miaka miwili.
Kulikuwa na jambo moja ambalo halikubadilika kwake kwa muda mrefu, alikuwa akisimama kwenye mlango kwa uangalifu, akingojea shambulio.
Tulimwekea Biblia ya sauti alipokuwa akicheza na kula, na kumruhusu atazame hadithi za Biblia kwenye TV – tulimjaza maandiko kimakusudi. Baada ya mwaka mmoja, kwa taratibu aliacha kukaa karibu na mlango akitazama; akili yake ilikuwa imebadilishwa na Neno la Mungu na alikuwa na amani zaidi.
Tafadhali, waombee watoto wa wamishenari waliouawa; kiwewe/trauma ni dhahiri na mahitaji yao ni halisi. Tunaomba kwamba kujitoa kwao kama dhabihu kwa ajili ya injili kutarudi kwa watoto wao kama baraka za Mungu juu ya maisha yao. Wengi wao wako nasi katika nyumba zetu za kimisheni zilizoko kote Nigeria.
-Sinmi, Compassionate Community Africa
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us