“Nia yao ilikuwa ni kuua” – nyakati za wamishenari

Tulijikuta kwenye mzozo wa kikabila wakati wa mkutano mmoja, ambapo kabila/kundi moja lilianzisha mapigano, likidai kuwa mmoja wa watoa huduma za afya alitoka katika kabila/kundi la watu ambalo walikuwa hawapatani na hilo kabila/kundi. Nia yao ilikuwa ni kumuua wakati watakapowasili kufanya hiyo shughuli ya huduma za afya, lakini kwa bahati nzuri watu wa Red Cross (Shirika la Msalaba Mwekundu) walipata taarifa hiyo na gari walilokuwa wakisafiria halikusimama kuruhusu mtu huyo ashuke karibu na watu hao waliokusudia kumuua! Chuki hiyo iliyokita mizizi ya kina ilitusababishia wasiwasi na kuzorotesha uwezo wetu wa kutoa huduma za afya kwa watu hao, lakini kwa upendo wa Kristo bila kujali hayo tulivumilia.
Licha ya magumu hayo, tulitiwa moyo wakati kundi la vijana lilionekana kutopendezwa na Imai ya Kikristo hapo awali ghafula lilianza kuonyesha udadisi kuhusu imani ya Kikristo na mara zote walikuwa na maswali mengi na kupenda kusimuliwa hadithi zaidi za Biblia. Hivyo, tulitiwa moyo kuendelea na kazi yetu ya afya pamoja na kumshuhudia Kristo kwa watu.
– Mfanyakazi wa Huduma ya afya, anayehudumu miongoni mwa jamii yenye makabila yenye Imani ya Kiislamu katika Afrika Mashariki.
Picha ya mwakilishi