Skip to content

“Ikiwa hawali nyani, basi hatuwezi kuwa na Mungu wao.” – nyakati za wamishenari

Musa alikuwa mtafasiri wangu; alitembea nami kila mahali, hata wakati nikiwa kwenye nyasi zetu za kuwinda. Yeye alikuwa akizungumza nami marazote, akiniambia wengine walikuwa wanasema nini. Kisha, siku moja, tulienda kuwinda, na hakusema neno. Je! nilikuwa nimefanya jambo la kumuumiza? Je, labda nilikuwa kwenye matatizo?
Jioni, aliniita. Alionekana mwenye huzuni na wasiwasi. Alichukua upinde na mshale wake na kunitaka nimfuate. Nilikuwa na wasiwasi, bila kujua ni hatima gani iliyoningoja, lakini nilihisi Roho Mtakatifu akiniambia nimfuate.
Tulisimama karibu na mwamba mkubwa mbali na kila mtu mwingine. Akasema, “Ndugu yangu, namtaka Mungu wako.”
Nilishtuka. Amemjuaje Mungu wangu? Sikuwa nimemhubiria kwa muda wa miezi mitano niliyokuwa naye huko!
Nilitaka kuwafikia Wahadzabe kaskazini mwa Tanzania. Wao wanaishi kwa kuhamahama na inasemekana kuwa vigumu kuwafikia kwa sababu ya mtindo wao wa maisha na uadui. Nilijua walihitaji mtu wa kuishi kati yao na kuwashirikisha ili waweze kumwona Kristo. Nilizungumza na kanisa langu la mtaa na wakapata maono haya na shauku, na kunituma kuishi miongoni mwa Wahadzabe.
Kwa muda wa miezi 5, nilikaa bila kushirikisha injili; kuishi kati yao, kuwinda msituni, na kujifunza jinsi ya kurusha mishale. Walinilinda katika uwindaji wetu. Walinizoea. Asubuhi moja tulipokuwa tukijiandaa kuwinda, nilitoa taarifa na kusema, “Namshukuru Mungu.” Kijiji kizima kiliahirisha uwindaji; walikuwa na wasiwasi sana. Kwao, hii ilikuwa ishara mbaya. Nilifanya jambo la kujifunza njia zao.
Nilikula vitamu vyao – tumbili na nyama ya kobe – na kuchimba maji kutoka kwenye chemchemi za chini ya ardhi pamoja nao. Baada ya muda, ilihitimishwa kuwa lazima niwe mmoja wao, Muhadzabe ambaye alikuwa amepotea na sasa akarudi kwao. Mimi ni kabila la Mhaya. Kisha Musa, mtafasiri wangu, akawa muumini.
Alisema wamekuwa wakinichunguza tangu nilipofika. Alikuwa akilia tukizungumza.
“Watu wengi wamekuja na kutuhubiria. Hatukukubali kwa sababu hawanywi maji yetu au kula chakula chetu. Walileta chakula chao na maji yao. Ikiwa hawali nyani, basi hatuwezi kuwa na Mungu wao.”
Wahazdabe pia walihisi hawapendwi kwa sababu wamishenari wengine wangeleta mahema yao badala ya kuishi katika nyumba zao. Nilivunjwa kwa ajili yao. Siku hiyo Musa aliamini. Injili ilipenya kijijini na Musa alikuwa muhimu katika kuhubiri.
Sasa tuna kanisa linaloweza kutumika, na Musa ndiye mchungaji wake.
-Kelvin Mshema, Tanzania, Mhaya mmishenari kwa Wahadzabe
Picha ya wawindaji wa Hadzabe na Andreas Lederer
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us