fbpx Skip to content

“Nataka kurudi mafunzoni na kufundishwa”- nyakati za wamishenari

Kijana kutoka chuo kikuu kimoja ninachohamasisha, hivi majuzi alimaliza digrii yake ya haki za binadamu na maadili. Ana shauku juu ya kazi ya uinjilisti; amekuwa akifanya uinjilisti akiwa chuoni na kijijini kwao. Mwaka jana, alifanya kozi ya Kairos ambayo ilimfungua macho kutambua makundi ya watu ambao bado hawajapokea injili; hili lilimpa shauku moyo wake huku akiendelea nalo katika maombi. Baadaye, tulienda naye katika safari ya kumtia hamasa hadi Kaabong. Tukiwa safarini, ilikuwa wazi kwake kwamba kweli kuna watu huko nje wenye uhaba wa kusikia injili ikilinganishwa na alikokuwa anatoka ambako makanisa “yanaongezeka kila siku kila mahali” (maneno yake). Nakumbuka alisema kwamba anahitaji kuweka kipaumbele chake ili kuzingatia wale wasiomjua Mungu. Ni mwaka sasa umepita.

Mwezi uliopita, alinifikia na kusema “Nataka kurejea shambani na kufunzwa, nikiwa tayari kushiriki injili mahali ambapo kuna uhitaji mkubwa wa watenda kazi na kwa watu wanaongoja kusikia habari njema na kufunzwa. Kwa wale ambao si wa utamaduni na lugha yangu kwa sababu hawa pia Mungu anawajali.” Wakati huo, nilimsifu Mungu kwamba anajitwalia kijana; Pia nilifikiri ingekuwa changamoto kwa kijana huyu aliyejawa na shauku na bidii kupata msaada wakutosha ambao ni endelevu kutoka katika kanisa lake. Mwezi huu, nitakuwanikishirikiana na kanisa lake la Rukungiri kumpeleka huku akijiandaa kuunganishwa na wamishenari kwenye jukumu/kazi kwa muda wa miezi sita huko Kaabong kwa ajili ya kuandaa, kujifunza na kutazama alipokuwa anajiandaa kutumika kwa muda mrefu.

Omba kwamba Mungu aweke shauku na moto uwakae katika maisha ya kijana huyu kufanya mapenzi ya Mungu kama mjumbe wake. Ombea kanisa lake la nyumbani, marafiki na familia kumuunga mkono katika safari hii huku akiitikia wito wa Mungu juu ya maisha yake. Niombee nipate kibali ninaposhirikisha kanisa lake, na kwa ajili ya maandalizi yenye mafanikio. Ombea kwamba miezi sita atakayokaa shambani/mafunzoni kujitayarisha kuwa mmishenari kutamsogeza karibu zaidi na Mungu na kusadikisha imani yake pia, na kwamba mafunzo haya yatakuwa na matokeo katika maisha yake. Ombea wamishenari wanaowakaribisha watumiwe na Mungu huku wakiwafundisha vijana kwa uaminifu mafunzoni.

Lynn, mhamasishaji nchini Uganda

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us