“Uso wa Musa ulikuwa umebadilika kabisa” – nyakati za wamishenari
Tulikutana na Musa* katika siku zetu za awali za huduma na tukawa marafiki wazuri. Mara nyingi tulimkaribisha nyumbani kwetu kupata chai. Chai iliambatana na mazungumzo kuhusu dini na maisha kwa jumla.
Siku moja alipita na kutukuta tunatazama video ya “More than Dreams”, ambayo ni mkusanyiko wa hadithi za jinsi baadhi ya Wakristo kutoka katika asili ya Kiislamu namna walivyokutana na Yesu.
Musa alitazama pamoja nasi japo kwa mshangao. Hakusema neno. Alichukua chai yake na kuondoka.
Jumamosi moja jioni baada ya chakula cha jioni, alianza kuongea huku macho yake yakiwa yametazama chini. Alisema amekuwa akitazama maisha yetu na hizo clips za video na sasa alitaka kumfuata Yesu.
Nilimuonya adhabu anayoweza kupata kwa kuukana Uislamu. Alinitazama na kusema, “Wacha hili libaki kati yako na mke wako”.
Alikuja kututafuta siku iliyofuata na akatuambia Yesu amemtokea usiku ule na alizungumza naye.
“Musa* mwanangu, unaanza maisha mapya. nitakuwa pamoja nawe na kutembea nawe. Sitawahi achana na wewe. Nitakuwepo kwa ajili yako daima. Usiogope wala hofu ya maisha yako.”
Naye Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa.
Uso wa Musa ulikuwa umebadilika kabisa. Furaha yake ilikuwa haina mwisho. Alitukumbatia sote. Kila aliyemfahamu alimuuliza aeleze nini kimempata.
Tumeona Mungu akimtetea huyu kaka katika magumu na mabaya. Alipoteza kazi yake mara moja baada yakutoa maisha yake kwa Yesu. Alikabiliwa na kufukuzwa kwa nguvu kutoka kwa boma na ndugu zake. Ndugu zake hata walikodi wahuni wamuue lakini alitoroka kimiujiza. Wamejaribu kila njia kumuondoa bila mafanikio. Bado amesimama na kuwafikia wengine katika mji wake.
*Sio jina lake halisi.
Imesimuliwa na Swahib Fathi, mmishenari.
Picha ya mwakilishi na Hadithi za AIM