“Ningeenda Wapi?” – nyakati za wamishenari

Jamaa mmoja mtaani kwetu alikuwa amesimama sehemu moja akiuza vitu kila siku, lakini hakuwa na mafanikio yakutosha. Aliweza kuuza labda kitu kimoja kwa siku. Baada ya kuishi huko karibia miaka 3, hatimaye nilimuuliza kwa nini hakuenda mahali pengine ambapo labda yeye angefanikiwa zaidi kuuza bidhaa zake. Alijibu kwa kuinua mabega akisema “ningeenda wapi?” Nilimsihi afikirie mabadiliko, nikimuuliza jinsi anaweza kuridhika kwa kuuza kitu kimoja tu kila siku? Lakini, alikuwa ameridhika kuketi pale alipokuwa.
Ilikuwa ni namna tofauti ya kufikiria kwangu, tofauti sana na mawazo ya nchi ya nyumbani kwetu!
-Mmishenari wa Afrika Kusini – Madagaska
Picha ya mwakilishi na hadithi za AIM