fbpx Skip to content

“Rafiki huyu mwaminifu” – nyakati za wamishenari

Nina rafiki mwaminifu. Tumefahamiana kwa muda mrefu sasa. Tulisoma shule moja ya sekondari (nilikuwa mbele yake mwaka mmoja) na tulikuwa tunakaa nyumba/hosteli moja. Baadaye tulienda chuo kikuu kimoja. Nilipoenda kufanya umishenari mara ya kwanza, aligundua kwamba nilikuwa nikihudumu kama mmishonari kwa sababu nilizoea kuchapisha vitu tulivyokuwa tukifanya, kama vile changizo la pesa kwa ajili ya kununua pikipiki. Bado alikuwa shuleni. Alipomaliza shule mnamo 2020 na kwenda nje kwa utumishi wa umma/taifa, alianza kuniunga mkono kwa asilimia 10 ya pesa zake kutoka katika utumishi wa umma kama zaka.

Baada ya utumishi wake wa kitaifa, alianza kufanya kazi katika kampuni moja kubwa nchini Ghana, na ameendelea kutoa zaka. Alikuwa ameona tulichokuwa tukifanya na alitiwa moyo sana. Baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja, tuliomba pamoja na akapewa miaka mingine miwili. Tangu wakati huo, amekuwa mwaminifu kwa kunitumia asilimia 10 ya mshahara wake na hunipa kila mwezi mfululizo. Kando na hili, kila inapofika siku yake ya kuzaliwa yeye pia hupanda mbegu maishani mwangu, akinipa kitu kwa ajili ya watu ninaofanya nao kazi, kama vile kufanyia timu ya soka sherehe ndogo.

Hakujawahi kuwa na mwezi ambao hajaunga mkono. Kwangu mimi, kuacha shahada yangu na kufanya hivi kwa muda wote haukuwa uamuzi rahisi, na jambo moja ambalo litamtoa mmisionari nje ya umishenari ni ukosefu wa fedha. Lakini kwa sababu ya uaminifu wa rafiki huyu, nimehisi kwamba Bwana ni Mpaji.

Reagan, mmishenari huko Kaskazini mwa Ghana

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us