“Ninyi ndiyo wenye hasara” – nyakati za wamishenari
Nilikuwa nikizungumza na mzee wa kijiji kuhusu jinsi walimu wanavyokatishwa tamaa kwamba watoto hawaendi shule. Nilieleza kwamba walimu wanajinyima sana kuja kufundisha watoto wa kijijini, na wamesafiri kutoka mbali na kujitolea kuacha maisha yao ya mjini. Ilikuwa ni aibu kwamba jamii haikutumia fursa hiyo kupata elimu, ikiashiria kuwa ni hasara kwao kama jamii ya wenyeji.
Mzee huyo alijibu hilo kwa kusema ni hasara kwa walimu kwa sababu ni wao ambao wamefika kutokea mbali kufundisha na hawana wanafunzi wa kufundisha. Pole sana kwa walimu. Nilishangaa sana!
-Mmishenari huko Tana River, Kenya