“Tuliomba na kuondoka; mbegu ilipandwa”- nyakati za wamisionari
Nimekuwa nikifundisha wanawake kanisani kwa miaka mingi na mwaka huu tumeanza kwenda kueneza injili kwenye jamii ya watu wenye hali duni. Nyumba nyingi zilitupokea vizuri. Tulikutana mwanamke mkristo ambaye alikuwa akiomba kwa Mungu watu wamtembelee. Alikuwa kaolewa na mwanaume Mwislamu alikua akimpiga kila alipotaka kwenda kanisani. Pia tulitembelea nyumbani kwa mganga mmoja aliyetukaribisha, na pia tuliwatembelea wanawake wanaouza pombe za kienyeji na kadhalika.
Hatukuruhusiwa kuingia nyumba zingine ambazo wamiliki wao walikuwa ni Waislamu, lakini wapo wengine waliotukaribisha na tukaweza kuwahubiria, japokuwa bado wamepofushwa na mafundisho ya dini yao. Tulifika kwenye nyumba moja na kumkuta kijana akifagia uani. Alikuwa anamalizia kufagia, lakini ni kana kwamba anatoa uchafu ili tufike pale. Tulipofika hapo, alitupatia viti. Tukamwambia, “Sisi ni wajumbe wa injili ya Yesu” naye akatuambia, “Nimekuwa nikiungojea ujumbe huu kwa muda mrefu.” Moyo wangu uliruka kwa furaha; tulimshirikisha injili na kumsomea maandiko, tukampa vitabu vya Injili vya Mataifa Yote na maandiko asome, akatuambia shangazi yake ana Biblia. Mwisho wa mazungumzo yetu, alituambia kwamba yeye ni Mwislamu lakini alihitaji kusikia ujumbe wa Yesu. Tukaomba nae na kuondoka; mbegu ilipandwa na tunaomba kwamba Roho Mtakatifu afanye kazi ndani ya mioyo ya wale waliosikia neno, hata wale ambao walikataa.
-Connie Arão, Mmishenari kutoka Afrika Kusini nchini Msumbiji