fbpx Skip to content

“Mishtuko ya kitamaduni ndani ya mambo ya ndani”

Kutumwa kutoka kwenye shule ya umisheni hadi shambani kwa mara ya kwanza, sita kati yetu tulisafiri toka kaskazini mwa Jos kwa masaa 8, halafu mbali hadi ndani ya msitu ili kulifikia kabila ambalo lilikuwa halijafikiwa bado la Kamuku. Huko, timu ilivuka mto kwa miguu kabla ya kuchukua baiskeli hadi kituo cha umisheni. Tulipowasili, timu iligawanywa na mimi na mwenzangu tulipanda baiskeli nyingine zaidi kuelekea kwenye nchi kavu, tukavuka mto mwingine kwa mtumbwi na hatimaye kupanda mlima.

Tulikutana na wenyeji ambao tayari walikuwa wamehubiriwa na ambao walitutambulisha kwa jumuiya. Walionekana kuwa wamepewa taarifa ya utume wetu na jinsi ya kushughulikia jambo hilo, kwa sababu tuliona kwamba mara baada ya kututambulisha,walijiondoa kimya kimya ili wasitupe nafasi ya kuondoka nao na kuwakataa watu!

Mshtuko wangu wa kwanza wa kiutamaduni ulikuwa mtoni, ambapo mabinti wawili wa umri wa miaka 15 hadi 17 walikuja wakitokea mtoni na kututazama kwa udadisi. Tuliaibika kwa sababu walikuwa vifua wazi, na tulipojaribu kuficha nyuso zetu, walionekana kushangazwa na haya yetu. Baada ya kuishi miongoni mwao kwa muda wa wiki 6 tukifanya huduma, tuligundua kwamba mabinti wadogo walijivunia kuonyesha matiti yaliyosimama kwa wanaume, na wengi wao huvaa ngozi za wanyama tu zilizofungwa kiunoni. Wanaishi katikati ya mashamba ya mahindi ya guinea na mahindi, na pia maharagwe, karanga na bamia. Hawa tuliwafurahia sana kwa sababu walikuwa wakarimu sana kwa eneo la chakula. Kila asubuhi hazikupungua sahani saba za milo tofauti-tofauti zilizowekwa kwenye mlango wetu. Hawazungumzi sana kihausa zaidi ya Kamukanci;hivyo, tuliwafikia kwa Kihausa kwa kutumia mmoja wa watu wao aliyetafsiri kwa kujitolea. Hatukujisumbua kujifunza lugha yao kwa umakini kwa sababu tungekaa kwa majuma 6 tuu; hata hivyo tulijifunza mambo ya msingi.

Itaendelea: juma lijalo, mikutano isiyofurahisha zaidi pamoja na azimio zuri.

-Kaka Ugochukwu G.U. ni mmisionari toka CAPRO akiwafikia waislamu wahamiaji wa kaskazini walioko m ashariki mwa Nigeria.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us