fbpx Skip to content

“Asante kwa lipi?”- nyakati za wamisionari

Hakim alinitazama bila msaada huku nikiendelea kusalimia watu kwa furaha: “Wamasanta hai!”

Hakim ni mkimbizi wa Kisomali anayeishi Kampala. Mnamo mwaka 2019, tuliamua kufanya tathmini ya mahitaji ya jamii miongoni mwa wakimbizi wa kisomali mjini Kampala ambayo ilijumuisha madodoso ambayo yalichukuliwa toka nyumba kwa nyumba. Hii ilihusisha kuorodhesha baadhi ya watafsiri wa kisomali kwenda nasi katika kila nyumba. Nilimwomba Hakim anisindikize kwa vile tayari nilikuwa nimejenga naye urafiki kwenye michezo ya soka ya ndani na darasa la kiingereza. Siku nzima, niliendelea kumsikia akianzisha mazungumzo na “Setahai” na “Wamasanta hai” akimaanisha “habari” na “asante” kwa heshima. Mwisho wa siku pia nilipata ujasiri na kuamua kuwasalimia pia watu tuliowaendea…ijapokua nilichanganya maneno. Nilisema moja ambalo lilimaanisha asante. Ningemwendea mtu na kusema kwa shauku, “Wamasanta hai.” Kisha mtu huyo angenionyesha sura ya mshangao. Kwa bahati mbaya, nilifikiri lazima watashangaa ninajua kisomali! Baada ya kufanya hivyo kwa mara kumi, mwanafunzi wangu Hakim alikusanya ujasiri wa kutosha kuniambia nilichokuwa nikifanya. Tulicheka sana juu ya hilo!

-Derrick, mmisionari wa muda mfupi miongoni mwa wakimbizi

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us