“Pizza na aibu”- nyakati za wamisionari
Waafrika Kusini, wanapomwalika mtu kwa ajili ya chakula, wanatarajia kulipia chakula hicho, na kinyume chake. Tulikuwa na baadhi ya Waamerika Kusini katika timu yetu ya tamaduni mbalimbali. Mara moja walinialika Kwenda kwenye pizza, na wakanihimiza kuagiza kwa kila mtu. Hata hivyo, mwishoni mwa mlo walitazamia nilipe sehemu yangu. Nilijisikia kuiabishwa sana kwani sikua nimebeba pesa za kutosha kwani nilifikiri wangenilipia!
Kutoka upande wa Madagaska, siku moja nilipokuwa nikienda kwenye ofisi ya serikali kusahihisha karatasi zangu, watu fulani wa Madagascar waliniuliza ikiwa wangeweza kuja kwa teksi. Nilikubali, na wakati wa kulipa ulipofika, kila mtu alikuwa akinitazama, akitarajia nimlipie nauli. Nikauliza nilitegemewa kumlipia kila mtu, wakasema ndio, kwa vile wanakuja kunisaidia katika biashara zangu, basi lazima nilipe kwa ajili ya kila mtu!!!
-Mmishenari wa Afrika Kusini nchini Madagaska