fbpx Skip to content

“Ufadhili wa ajabu wa Mungu” – nyakati za wamisionari

Kwa miaka kadhaa, nilikuwa nikifanya kazi miongoni mwa wakimbizi wa Kisomali, na nilitumia ofisi iliyokua kwenye kiwanja chetu cha kanisa kuwafundisha wanawake ujuzi wa ushonaji huku nikijenga urafiki na kushirikisha upendo wa Mungu. Wakati fulani, kujikimu kwangu ulikuwa wa chini sana na nilipata miezi tisa nyuma ya kodi ya pango, iliyolipwa kwa kanisa, na walinitumia barua wakinitaka nilipe kiasi chote ndani ya juma moja.

Nilihisi kuvunjika moyo na kufadhaika, na nikamwambia Mungu, huku nimeshikilia barua ya mahitaji ya kodi mikononi mwangu: “Mungu, sikujiita kwa kazi hii, uliniita. Kwa hiyo ikiwa nitafedheheka, ni wewe unayepata fedheha, si mimi. Ikiwa uko tayari kwa fedheha .Binafsi nitaendelea kufanya kile kilichonileta hapa. Kwa maneno hayo ya hasira, niliihifadhi barua na kuendelea na kazi yangu ya siku hiyo.

Siku hiyo hiyo, kanisa lingine liliniita na kuniuliza nimsaidie mwongofu mpya toka uislamu, ambaye alishirikisha hadithi za kutisha za kutupwa nje ya nyumba yake na kukosa chakula baada ya kubadili dini na kuingia kwenye ukristo. Tulimpigia simu ndugu mmoja katika shirika linalosaidia watu kama hao, na kwenda kumwona. Ofisini kwake, alitoa pesa za kusaidia, kisha akanitazama na kuniuliza nina shida gani. Nilishangaa kwa sababu sikuwa nimesema chochote kuhusu tatizo langu, lakini nilimshirikisha. Alisema, “Njoo juma lijalo kuchukua hundi.” Huu ulikuwa muujiza – andiko lilikua kubwa!

Ni kwa namna gani inashangaza Mungu alitumia hali nyingine kunileta niwasiliane na mtu huyu ambaye nilimuona mara chache sana, ambaye alinipa msaada niliohitaji. Katika nyakati hizo maishani haujui namna gani ya kuomba, Wakati wote yeye ni mwaminifu na yupo tayari kusaidia. Wito wa Mungu maishani mwetu ni wajibu wake kutulinda, kwa hiyo msemo usemao, “Palipo na maono, pana riziki.” Nimemwona Mungu akipitia kwa ajili yangu kwa njia nyingi za miujiza ambazo zimethibitisha wito wangu kila wakati na kunitia moyo kuendelea. Vinginevyo, ningeacha zamani! Kuwa mmisionari wa Kiafrika sio jambo rahisi kwa sababu kutafuta msaada bado ni changamoto. Daima ni safari ya imani.

– Mmishonari wa Kenya

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us