fbpx Skip to content

“Upepo ulioganda“- nyakati za wamisionari

Tulitoka Kaskazini mwa Kenya kufanya mafunzo ya misheni, na tukasafiri hadi sehemu nyingine kufanya ushuhudiaji. Tulikaa siku nzima katika eneo lenye upepo mwingi, tulienda mlango kwa mlango kwenye kijiji kizima, tukipanda juu na kushuka chini na kuzunguka katika hiyo hali ya hewa.

Jioni ilipokaribia, tuliweka vifaa vya kuonyesha filamu ya Yesu lakini upepo ulianza kuwa mwingi. Vifaa vilianguka kwa mara ya kwanza, mara ya pili, mara ya tatu, lakini hatukufikiria kuhairisha kwa sababu tulikuwa tumetumia siku nzima kuwaambia watu waje kuona. Tulikuwa tumewaambia kwamba Yesu angezungumza kwa lugha yao, kwa hiyo walikuja kwa wingi na walikuwa wametembea umbali mrefu katika hali hiyo mbaya ya hewa ili tuu kuhudhuria.

Hatukuweza kupata vifaa vya kukaa juu katika upepo huo, hivyo hatimaye tukaamua tungeshikilia nguzo zilizoshikilia skrini. Kulikuwa na upepo mkali na baridi kali, na tulijitahidi kuvumilia kwa karibu masaa mawili na nusu. Filamu hiyo ilionekana kuwa ni ndefu zaidi kuwahi kuonyeshwa! Hatimaye mmoja wetu alichoka sana na akaanguka chini. Lakini tulihisi lazima tuendelee, ingawa tulikuwa tumetembea siku nzima.

Mmoja wa wanakijiji waliokuwa wakitutembeza mchana alikuwa akitusihi tusiache, akisema, “Jamani, watu wamekuja!” Alikuwa anatueleza kwa nini tuendelee.

Tulivumilia, na mwisho wa filamu, watu 20 walitoa maisha yao kwa Kristo! Siku iliyofuata watu walikuwa wakisimulia habari kuzunguka kijiji kuhusu sinema na jinsi Yesu alivyokua akiongea lugha yao. Na waliendelea kuzungumza juu ya “watu hao walioshikilia skrini wakati wote!” na walishangazwa.

Uzoefu huo unaifanya kuwa juu ya orodha ya matukio ya ajabu ambayo nimepitia kufikia sasa.

-Mmisionari wa Kenya

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us