“Mkate wa kahawia na supu” – nyakati za wamisionari
Wakati Watoto wangu watatu walipokua wadogo sana, mume wangu na mimi tulijiunga na timu ya umisionari kwenda Namibia na Afrika Kusini. Kulikua na vijana 25 waliotembea pamoja nasi,na katika maeneo mbalimbali tuliokaa, yalikua hayafurahishi kabisa kwa uwepo wa choo kimoja tuu!
Tuliendesha kwa muda mrefu na tulitembelea majiji mengi na miji, tukihubiri Injili. Kuna wakati Watoto walikua wanahangaika, na vijana waliona ngumu kuchukuliana nayo. Mara kwa mara tulikosana. Safari ilionekana itadumu milele, na nilijikuta kwenye turubai wakati wa mvua kubwa iliyokua ikinyesha na tulifika tukiwa tumechoka watoto wakamuuliza Mungu , nini kwenye dunia hii, nilichokua nafikiria kuja kwenye safari hii! Jambo la kwanza, boksi letu dogo lililokua na pesa taslimu liliibiwa na tulitumia siku zilizobaki kwa kushindia mkate wa kahawia na pakti za supu, matumbo yetu yalikua yakiunguruma.
Ijapokua , kwenye mapumziko mafupi, mmoja kati ya wanajumuiya kwenye timu yetu alivunjika mguu wake na ilimpasa aweze kumuona tabibu na kutibiwa mguu wake. Viongozi waliamua tukae kwenye mji huu kwa muda mrefu na wakulima waliokuwepo walituhudumia vizuri, walituhudumia kwa vyakula vizuri na kutujali. Mungu alijua tulihitaji kuinuliwa!
Safari ya umisionari ilikua mara kwa mara yenye majaribu ya kuumwa, lakini watu walikuja kumjua Yesu na tukamshukuru Mungu kwa maisha yao na utoaji wake.
Hakutupa ahadi ya dunia pasipo matatizo, lakini anatujali na tunashukuru tuliweza kutumika.
-Mzimbabwe kwenye umisionari wa muda mfupi