fbpx Skip to content

“Kucheka na watakatifu” – nyakati za wamisionari

Kutumika kati ya watu kwenye muhktadha wa tamaduni zilizo kinyume na wako inaweza kuvutia na changamoto, wakati mwingine kuaibisha na kukera! Nilipatwa na hali ya Ngozi kuvimba nikiwa kwenye mkutano wa wachungaji ndani ya Minembwe , Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Nikiwa sehemu ya wazungumzaji, tulitegemea wenyeji kutafsiri tulipokua tunawasilisha kutoka lugha ya kiingereza kwenda kinyamulenge. Tulikua tumerudi kutoka kwenye mapumziko ya chai na ilikua zamu yangu kuzungumza.

Nilikwenda kwenye mimbari kwa kujiamini ili kuanza, lakini nilikua sijui, mtu aliyepaswa kufasiri alikua hapatikani. Niliomba na kuanza mkutano kwa kuwasalimia Muraho neza ( habari zenu). Kulikua na mwitikio wa sauti kubwa kutoka kwa washiriki na walinikodolea macho kwa mshangao wa ghafla kwa kuzungumza lugha yao na niliganda kwa aibu. Waliponitazama usoni, walinicheka kwa nguvu zaidi!Nilionekana kituko, nilimtafuta mtafsiri wangu pasipo kumpata, halafu ghafla akakimbilia ndani. Nikajisikia vizuri na kuungana na kusanyiko kwa kicheko cha “raha takatifu”.

-Mmisionari mnaijeria nchini DRC

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us