fbpx Skip to content

“Nafsi zinapotea!” – Nyakati za wamisionari

Inaelezewa hadithi ya mwanamume mmoja muungwana ambaye alikuja kumjua BWANA na alijifunza kuhusu agizo la BWANA ili kuweza kuvuna nafsi kwa ajili yake. Alikua na msukumo mkali katika kua mtii na alishangazwa kuona waamini wengi walipoteza muda kwenye vitu ambavyo alifikiria kuwa havina maana. Angeweza kuja katikati ya kundi la wapendwa wakitazama luninga na mikono yao ikiwa kiunoni na katika mfadhaiko, angesema, “ Wapendwa, nafsi zinapotea na mmekaa hapa mkitazama luninga”. Washirika walimualika kwenye mazungumzo na aliwarudishia maneno , “Nafsi zinapotea na ninyi mnapiga soga!”. Na wakati rafiki zake walipochukua muda mrefu ili kuwa tayari, angewaambia, “Rafiki, nafsi zinapotea na umetingwa kuchana nywele zako!” Huu ulikua msukumo wake kwenye kuvuna nafsi na aliwavunja moyo wengine ambao wasingeonyesha hili kwa haraka, habari hii ilisambaa kwenye jamii yake; “Nafsi zinapotea” na aliwasha moto wa kueneza Injili.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us