fbpx Skip to content

“Salama salimini kabisa!” – Nyakati za wamisionari

Nilikuwa mmishenari mpya nchini Afrika Kaskazini, nikiishi nyumbani kwa wafanyakazi wenzangu. Walitoka kwenda mji wa mbali, nikabaki peke yangu na nikashikwa na woga na wasiwasi. Nikawa naenda nje kuangalia geti, kuhakikisha kuwa kila kitu kilikuwa salama usiku huo. Nilipotoka nje ya mlango wa mbele, ulijibamiza na kujifunga nyuma yangu, nikawa nipo mbele ya nyumba kati ya mlango wa ndani na geti dogo la mlango. Geti hilo na mlango, vilikuwa vimejengwa na kufungwa kwa uimara na usalama.

Sikuwa najua Kiarabu hata kidogo, na nilijua kwamba ningelazimika kuakaa hapo kibarazani mbele ya nyumba kwa siku kadhaa mpaka pale wenye nyumba watakaporejea. Badae nikaona majirani katika wamekaa nje wakila, nikawa sina budi ya kuwaomba msaada! Ikanilazimu tu nizungumze Kiingereza, lakini walinipuuza kwanza lakini baadae ndiyo wakaamua kunisaidia hivyo hivyo, bila hata ya kunielewa nilichokuwa naongea. Ilibidi wampigie simu mdada wa usafi wa pale nyumbani, ambaye alikuwa na ufunguo wa nyumba, lakini hata hivyo ilibidi tuvunje dirisha ndiyo tuingie ndani ya nyumba. Nilijihisi mnyonge sana lakini nilishukuru kwamba mwishoe walitambua tatizo langu na kunisaidia kutoka katika kifungo changu hikil!

-Mmishenari wa kutoka Afrika Kusini mpaka Afrika Kaskazini

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us