“Vijana wenye hasira” – Nyakati za wamisionari
Tunafanya kazi katika kundi la watu wa Kiislamu, na tumepata baadhi ya waongofu. Familia zao na viongozi wa eneo hilo hawakupendezwa sana na jambo hilo na hata sisi tulihofia maisha ya mmoja wa waongofu hawa. Tulianza kusikia kuhusu mashambulizi yaliyopangwa kufanywa dhidi ya nyumba yetu, na hatukuwa tunalala kwa amani kwa muda mrefu kwa sababu ya wasiwasi wa kushambuliwa saa yoyote.
Siku moja, kundi la vijana hao walipanga kutushambulia. Tulienda kituo cha polisi na viongozi wao wakuu waliitwa. Lakini hata hivyo kwenye baraza kuu la mfalme wao, tulipewa ruhusa ya kuwahubiria watu wenye umri wa miaka 20 na zaidi! Haki hii iko kwenye katiba ya nchi hiyo, na wao walilitambua hilo. Hivi sasa huduma itakuwa rahisi zaidi kwetu, na kwa wamishenari wengine. Viongozi wakuu waliitisha mkutano wa kuturejeza kwenye jamii hiyo na kutoa onyo kali kwa yeyote atakayethubutu kutushambulia. Mungu asifiwe!