“Faragha tafadhali!” – Nyakati za wamisionari
Tukiwa wamisionari wapya wa shambani mwa BWANA, tuliwekwa pamoja na familia ya wenyeji ili kuutazama utamaduni wao. Baba alizungumza kiasi Kiingereza, na akatoka nje na mume wangu kwa muda. Mama, ambaye hazungumzi Kiingereza, aliniacha nyumbani na binti yake, ambaye pia hazungumzi Kiingereza, nami sikufamu lugha ya wenyeji. Kabla hajaondoka ni wazi alimuagiza binti akae nyumbani.
Mara tu baada ya mama alipoondoka, binti alianza kwenda nje na nilihisi kuwajibika, nilijaribu kumzuia asiondoke. Alisisitiza kwa nguvu, na alipotoka nyumbani, nilimfuata. Hakuwa na furaha juu ya hili na akaniashiria kwa haraka: “rudi nyuma, rudi nyuma!” lakini niling’ang’ania.
Hatimaye, alikuja karibu, akanitazama usoni, kisha akachuchumaa kwa kumaanisha. Maskini msichana alihitaji kwenda kujisaidia na nami nilishindwa mruhusu afanye hivyo kwa faragha! Nikiwa mwenye uso wa aibu , nilirudi nyumbani, naye akarudi ndani ya dakika chache.
Mama aliporudi nyumbani, msichana huyo alimwambia mama yake kilichotokea, nao walitaka kuanguka kwa kicheko. Nilishindwa kujizuia hivyo nikajiunga nao na miaka ijayo, hiyo familia na mimi bado tunataniana kwa kutokuelewa kwangu, kila mara tunapokutana. Ninazungumza lugha hiyo kwa ufasaha sasa, na uzoefu ulinipa sababu nzuri ya kujifunza kwa haraka!
-Mmisionari wa Kenya nchini Sudan ya Ku