fbpx Skip to content

Tayari kwa ujenzi wa taifa

Kate Azumah & Furaha Kengela

Afisa mmoja kutoka Sekritarieti ya Jeshi la Kujenga Taifa alishindwa kubadilisha msimamo wa kuruta wawili. Kwa nini mtu ang’ang’anie kuwapeleka watumishi kwenye maeneo ya mbali vijijini wakati kuna nafasi bado kwenye maeneo ya mijini yenye huduma zote muhimu? Kuruta wengi wangekuwa tayari kulipa hata pesa kwa nafasi za mijini. Hata alifika mahali pa kufikiria kuwa vijana hao walikuwa ni wapelelezi. Michael na Eben walikuwa sehemu ya msururu mrefu wa wa mishenari waliokuwa kwenye orodha ya Mkakati wa Tumikia Ulimwengu (OSG). Wakati wa majuma sita ya mafunzo kwa wa mishenari wakazi, walikuwa wakiiombea sana jamii ya Builsa. MKAKATI WA KUTUMIKIA ULIMWENGU Mkakati huu (OSG) hufunza na kutuma vijana kama wamishenari kwenye jamii ambazo bado kufikiwa na injili wakati wanafanya wajibu wao wa Jeshi la kujenga taifa. Huko Ghana, kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ni lazima kwa wote waliomaliza mafunzo ya vyuo vya kati na vyuo vikuu. Serikali huwapeleka maelfu yao kila mwaka kutumika katika sekta mbalimbali kama ajira za kitaifa na kuwalipa posho kila mwezi.

MIRADI YA UFALME “Kile ambacho Mungu amekirahisisha, sisi tusikifanye kuwa kigumu,’’ anasema Mch. Sola Adebayo wa Miradi ya Ufalme wa Mungu unaoitwa The Kingdom Projects (TKP) nchini Nigeria. “Bwana hakusema, acha kazi yako na nenda ulimwenguni.’’ Alichosema, ni kwamba, “Nendeni ulimwenguni kote na kuihubiri Injili.’’ TKP imepata njia endelevu za kufunza wafanyakazi wanaolipwa na serikali kutumika kama wamissionari katika maeneo wanayopelekwa baada ya mafunzo ya kujenga taifa. Jamii iko tayari kuwapokea wamishenari wa namna hii, na kazi zao za serikali hufungua milango ambayo vinginevyo isingeweza kufunguka. Mbinu ya namna hii hupunguza mzigo wa kutafuta msaada binafsi. Chuo cha TKP cha watengeneza mahema huunganisha mafunzo ya umisheni kwa wale ambao huunganisha pamoja na kazi za serikali. Wamishenari waliofunzwa na TKP wamethibitika kuwa bora katika uinjilisti, ufundishaji wanafunzi na upandaji makanisa, uhamisishaji umisheni, umisheni wa matibabu ya binadamu, na shughuli za maendeleo ya jamii.

MWALIMU AMBAYE NI MMISHENARI NCHINI TANZANIA Iman ni mmishenari kutoka kijiji cha Mzenga wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, ni mzawa wa eneo hilo. Iman aliokoka mwaka 2011 na kuamua kwenda kufanya kazi kwa watu ambao bado hawajafikiwa na injili. Mwanzoni kabisa watu wa kabila hili walikuwa wagumu kumpokea na kumpenda lakini baada ya kuwaonyesha faida ya kazi ambazo zinawaletea fedha na chakula wakaanza kumpenda na hapo ndipo akaanza kufanya nao miradi mbalimbali. Kwenye Kijiji hiki Iman ameunda vikundi vinne vya kujifunza Biblia ambavyo hufundisha na kuzungumzia mambo yaliyo kwenye Biblia na kujibu maswali mbali mbali ambayo watu hujiuliza kuhusu Yesu na Mungu. Maswali kama “Je, Yesu ni Mungu au sio Mungu?” Siku za wiki Iman huenda kwenye kazi ya ualimu na mida ya jioni huenda kwenye huguli za kilimo na ufugaji ambazo hufanya pamoja na wanavikundi mbali mbali wa kijijni hapo. Kabla kuanza shuguli Iman aliwonyesha msingi na umuhimu wa kumtanguliza Mungu na hivyo na alifanya hivi ili iwe kaiwada ya wanakikundi hawa kuzoea, ili wasipate kutegemea namna mbadala au miungu mbadala katika shugh uli zao.

Iman anasema hakuna changamoto yeyote ile kwa upande wa kazi yake ya serikalini endapo tu atatimiza wajibu wake wa kazi anazotakiwa kufanya. Iman na mke wake walifunga ndoa mwaka jana (2022). Mungu alimpatia mtu sahihi ambaye anafanya nae huduma kwenye eneo hili. Hivi sasa wamebarikiwa kupata mtoto mmoja mwaka huu, lakini pia wanaishi na mama yake mzazi Iman ambae ana changamoto za kiafya kidogo hivyo yupo hapo wakimuhudumia Iman anasema umishenari hapo Mzenga unahitaji wito kutoka ndani na msaada wa Mungu. Mtu yeyote kwenye huduma kama hii anahitaji ajisimamamie mwenyewe, kuipenda huduma, bila kusahau kutilia mkazo kwenye kusoma neno na maombi.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us