fbpx Skip to content

Harbari na mafunzo

Kila mwezi Chuo cha umisheni cha Afrika Mashariki hutoa mafunzo ya umishenari kwa viongozi mbalimbali wa makanisa wakiwa ni wachungaji na wazee wa makanisa. Viongozi hawa wa makanisa hufikiwa kupitia kiongozi mkuu wa makanisa ya sehemu maalumu makanisa yalipo kwa kuwa yeye huwafahamu viongozi wote na huwaleta viongozi hawa pamoja na kuwapa/kusambaza taarifa hiyo. Mafunzo haya hufundishwa na Kelvin Mshema na viongozi wengine watatu, ambapo hufundisha mada 4 kwa muda wa siku 4 na mada zote na zipo kwa mtiririko kuanzia umisheni ulipoanzia na mpaka ulipo hivi sasa na mwisho wa siku wanajua kila kitu juu ya umisheni. Lengo kuu la mafunzo hayo ya umisheni ni kwa lengo la kuwajuza watu na pia kupata watu wengine wanne watakaosimama katika nafasi nne muhimu za umisheni; muombaji, mtumaji, mhamasishaji na mutumwaji. Wanapoanza mafunzo washiriki wote hupewa vitini vya somo husika la siku na kufuatilia kwa ukaribu kinachofundishwa kwa siku zote nne. Wanapomaliza mafunzo hayo ya umisheni huwa kuna vitabu vinavyouzwa kwa bei nafuu sana kuwasaidia zaidi watu hawa waliohudhuria mafunzo.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us