fbpx Skip to content

Tumeitwa tumeagizwa kuhubiri injili katika nchi za Afrika ya kaskazini

AfriGO team

Kufanya kazi katika Afrika Kaskazini inaweza kuwa ni hatari, na Daudi anajua hili vizuri. Polisi humfuata Daudi anakoenda; wakiwa na wasiwasi na uwepo wa Wakristo. Baadhi ya majirani zake humkejeli na hata wamekuwa wakimtishia kifo.

“Hapo mwanzoni ilikuwa ngumu sana, lakini sasa najua kuwa huwa nachunguzwa. Nimeishi kwa miaka minne kwa namna hii.’’ Hata hivyo, Daudi ana uhakika kwa kiasi fulani kuwa hata akikamatwa hatapigwa, lakini anaweza kufukuzwa nchini.

Uhakika wake kuwa jina la Kristo lazima lijulikane na ndiyo ujumbe uliomleta hapo.‘ Nilipokuja kwa Yesu, kumjua yeye ilikuwa moja ya vitu vikubwa nilivyovipata, lakini nilijifunza kuwa kuna mahali pengine ambapo hakuna makanisa kabisa na kwa hivyo hakuna mtu wa kuwaeleza habari za Injili.’ Daudi alitafuta mitandao kama vile ile ya Mradi wa Yoshua ili kujifunza zaidi. ‘Mungu alianza kugusa moyo wangu’ anasema Daudi.

Hatimaye, alihudhuria mafunzo ya umisheni na kuanza kutumika miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya huko Kaskazini, ambapo ni makanisa machache tu yanapatikana tena katika miji mikubwa tu lakini hakuna makanisa kwenye maeneo mengi. Daudi alibarikiwa kufanya kazi kwa muda na mmishenari mmoja na kushirikiana na makanisa ya wenyeji. Mahali anapoishi Daudi sasa, vijana wanataka kujua zaidi.

Polisi wanachunguza kanisa dogo na kuona ni nani huwa anakuja na kuondoka. Wakati mwingine wanaangalia vitambulisho vya wale wanaohudhuria kanisani. Polisi wanaweza kuwapa taarifa zao na wanaweza hata kupoteza kazi zao na hata marafiki. Wanafamilia ya mwamini mpya wanaweza kumpiga au hata kumkataa kabisa.

Kwa ujumla, Daudi anakutana kwa siri na wale ambao wanapenda kusikia habari za Yesu, ingawa hii bado ni hatari kwake. Aliwahi kukutana na mtu ambaye alionekana ana hamu ya kusikia habari za Yesu, lakini mtu huyo baadaye alimtumia ujumbe wenye vitisho vya kifo.

Kuwa mtu mweusi ni changamoto nyingine pia. ‘Kwa nyakati fulani husema mambo ya kibaguzi dhidi yangu. Ni vigumu hata kwenda madukani. Unapotaka kupanga nyumba, mwenyeji atakubali wakati mnaongea naye kwenye simu lakini ukienda kumwona anakukatalia.

Hata hivyo hali hiyo ni tofauti kwa wakristo. Daudi anaweza kukaa kwenye nyumba za wakristo kwa muda. Katika ushirika na wakristo, humtia moyo Daudi na hivyo kumpunguzia magumu ya maisha.

Tuliongea na Daudi muda mfupi kabla ya noeli, na kwa kweli alikuwa anasubiri kwa kusanyiko la wakristo kutoka sehemu zote za nchi siku hiyo ya noeli.

Alipoulizwa kama anajisikia vizuri kuwa na familia, Daudi alicheka. ‘’Baadhi ya wanawake katika kanisa langu la nyumbani wanasema hawawezi kuja hapa.’’ Akaendelea kusema, ‘ Lakini kama Mungu anamwita mmoja wao, basi tunaweza kuwa na familia hapa. Kuna changamoto, lakini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.’’

Ushauri wa Daudi kwa kijana mwenye wito kwa ajili ya watu ambao bado hawajafikiwa uko dhahiri : ‘’Nakushauri kuwa na kanisa linalokutuma. Hii ni muhimu sana.’’ Anasema kwamba anapoenda nyumbani, kanisa lake humpa muda wa kutoa ushuhuda, na kisha kumwombea na kumsaidia. Anapopata changamoto, viongozi humpa ushauri. Huu ni msaada wa thamani.

‘Vijana wengi wanataka kufanikiwa kufanya kitu kwa ajili ya Mungu, lakini wachache wanafahamu kwamba tunaishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Vijana wana hisia kuwa umisheni ni kazi nzuri, lakini umisheni ni kazi ya pole pole na ngumu. Daudi anavumilia na anaona matunda.

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us