fbpx Skip to content

Makundi ya Watu: Watoposa

Watoposa ni jamii ya wakulima na wafugaji wanaoishi Sudani ya Kusini, wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 500,000. Watu hawa wanategemea ng’ombe, kondoo, na mbuzi. Wavulana huchunga mbuzi na kondoo na huacha kuchunga ng’ombe wakifikia umri wa mkubwa. Wakati wa masika wanyama wanachunga karibu na vijiji. Mvua zinapokoma, wanaume hupeleka makundi ya mifugo kwenye maeneo malisho wakati wa kiangazi na huwarudisha mvua zinapoanza. Watoposa pia wanafanya shughuli ya kuchenjua dhahabu na madini mengine.

Kila tukio kubwa la kijamii huhusisha kutolewa kwa ng’ombe kama malipo au ahadi. Hali hii huweza kusababisha msuguano kati ya majirani pale ambapo hakuna ng’ombe wa kutosha kwa ajili ya mahari ya mke wa kwanza. Wanasifika kama watu wenye tamaa kubwa ya umiliki wa ng’ombe kuliko makabila jirani. Mtu ambaye anaweza kutoa ng’ombe wengi hasa kwenye kipindi cha vita, hupewa heshima ya juu.

Utawala wa kisiasa ndani ya watoposa hauko wazi, ingawa wazeee, machifu na watu wenye busara hupewa heshima. Maamuzi katika ngazi ya ukoo au jamii hufanywa kwenye mikutano ambayo huwa inahudhuriwa na wanaume pekee. Wanawake hubakia nyumbani kulima, kupika na kulea watoto.

Utamaduni wa Watoposa huendelezwa kwa njia ya mdomo kama nyimbo, ngoma, muziki, mashairi, na hadithi. Watoto wengi wa jamii ya watoposa sasa wanakwenda shule, lakini kiwango cha kujua kusoma na kuandika kiko chini.

Wanaweza kufikiwaje na injili?

Watu hawa wanaamini katika miungu na viumbe fulani kuwa vina uwezo kama vile roho za mababu zinasaidia matatizo yao ukame na milipuko ya magonjwa ya mifugo. Imani hizi zinaunganishwa pamoja na katisimu ya wakatoliki, pamoja na hirizi na imani juu ya dini zinazoamini kuwa watu wanakuwa kama walivyojaliwa na hawawezi kubadilika.

Idadi ya Wakristo Watoposa ni chini ya asilimia moja. Wamissionari wametumia mafunzo ya ufuasi na masimulizi ya Biblia ambayo yamekuwa yanatolewa na viongozi waliofundishwa. Watu wenye moyo wa utumishi pamoja na taaluma katika maeneo kama udaktari, mifugo, kilimo na maji wanatakiwa ili kuwafikia watoposa na injili. Wamishenari wachache kutoka Kenya wamekuwa wakifanya kazi huko.

Mwombe Mungu ili:

  • Atume wamissionari wenye ujuzi wa kilimo, udaktari na udaktari wa mifugo kuwapelekea watoposa injili.
  • Wawepo watafasiri ili watu wapate Biblia katika lugha zao za kwanza.
  • Atoe watendakazi wa injili ambao wana ujuzi katika kufundisha maandiko kwa njia ya mazungumzo.
  • Awasaidie Watoposa kuendeleza mahusiano mazuri miongoni mwao na majirani.
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us