Wameitwa: Tony Na Julia Mburu
Mungu anapokuonyesha anachofanya, ni mwaliko wa moja kwa moja kwamba anataka uungane naye. Maneno haya kutoka kwenye darasa la kujifunza Biblia yalikuwa ni ufunuo mkuu kwangu. Hata hivyo uamuzi wangu kufanya kazi kama mhamasishaji na mmishonari ulikuwa ni mchakato, si kama vile aya moja inavyotoka kwenye ukurasa wa Biblia. Nilijua kuwa nilitamani kumtumikia Mungu; lakini sikujua ni kwa vipi.
Tulipoanza kusikia wito wa Kimakedonia, tulikuwa bado hatujaoana na ulikuwa ni uamuzi mgumu. Nilikuwa tu nimemaliza masomo yangu ya uhandisi wa umeme na elekronikisi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, (Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology) wakati Julia alikuwa mwaka wake wa mwisho wa kusomea Teknolojia ya Habari. Tuliweka mipango kwa yale tuliyotaka kufanya. Hatukutaka kujihusisha na kazi ya Uhamasishaji kwa muda wote.
Tulifanya kozi ya KAIROS pamoja mwaka 2010, ilikuwa dhahiri nini nilitaka kufanya- kuhamasisha umisheni! Kupitia kozi hiyo, Mungu alitusaidia kushinda hali ya kuwa na hofu ya maisha. Tuliingia kwenye huduma ya muda wote pamoja na Mtandao wa Kampeni ya Umisheni [Mission Campaign Network (MCN)].
Kuhamasisha watu kwa umisheni ni sawa na kutabiri. Manabii waliita watu kurudi kwenye kusudi la Mungu. Kimsingi tunarudi kwenye kusudi halisi la kuishi kwetukueneza Injili hadi kwenye miisho ya dunia, kuwa kama Kristo, na kuunda Amani (shalom) katika nchi, miji na vijiji. Kuhamasisha siyo tu kwa ajili ya makundi ambayo hayajafikiwa, ingawa ndiyo hasa yanayopewa kipaumbele. Ni kuhusu kuona utukufu wa Mungu katika kila eneo la jamii.
Katika Agano la Kale, manabii wangeweza kupiga tarumbeta kuonya au kutoa ujumbe muhimu. Kama wahamasishaji, tunapiga tarumbeta kwa uwazi kwa kanisa na kutangaza kwamba ni wakati kwa Afrika kuinuka na kupeleka injili kwa ulimwengu. Katika MCN, tunahamasisha kanisa kuchangamka katika kufanya umisheni.
Kila mwamini anatiwa moyo kuhamasisha, kwenda kama mmishonari au kuwezesha watu walio tayari kwenda, wawe wanasaidiwa kama kusaidia kulea wamishonari au kama wanataaluma na watengeneza mahema. Pia tunasisitiza jukumu muhimu la maombi kwa ajili ya umisheni.
Mafunzo ya MCN huanza na semina fupi ya masaa mawilimatatu kuwaonyesha watu kwamba umisheni ni msingi wa Biblia. Tunasisitiza kile kilichokwishafanyika sasa na kile ambacho bado hakijafanyika. Tunashirikiana na kila sehemu ya mwili wa Kristo iliyo tayari na mashirika mengine ambayo yanayo shughuli kama za kwetu ndani na nje ya Afrika. Kozi zetu hazijatengenezwa na MCN bali na washirika wetu kama vile Simply Mobilizing International, the Center for Mission Mobilization, na Perspectives. Pia tunafundisha namna ya kukabiliana na ulimwengu wa Kiislamu.
Kutoka mwaka 2011 hadi 2018, tulifanya kazi Nairobi, Kenya tukiendesha kozi za KAIROS kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya 1000 na Makanisa.
MCN imekuwa siku zote ikitamani uhamasishaji kutokea huko Mombasa, mji ulioko pwani ya Kenya ambao wakazi wake ni nusu kwa nusu kati ya Wakristo kwa Waislamu. Wengi wao ni Waswahili na Waarabu. Wakristo wengi hawajui namna ya kuwafikia waislamu – hata hawajui kama wanapaswa kuwafikia. Tulialikwa kuanzisha uhamasishaji na tulikubali, tukaingia huko mwaka 2018.
Kwa kazi ya umisheni, na hasa kazi iliyobakia ya kuuhubiria ulimwengu, uhamasishaji ni kitu cha kimkakati kilichobakia kwa ajili ya uinjilisti kwa ulimwengu. Kanisa linahitaji kukamilisha kusudi la kuwepo kwake. Swali ambalo tungependa kila mtu kujiuliza ni hili, “Ni nini sehemu yangu katika umisheni?” www.missioncampaignnetwork.org