“Waliacha kututazama kama maadui” – nyakati za wamishenari

Mchungaji Edwin B. Fussi na familia yake walihamia kwa watu wasiofikiwa Tanzania, lakini walikumbwa na kukataliwa, kejeli, na kupungukiwa msaada wa kifedha kutoka kwenye makanisa yaliyowatuma waliposhindwa kupata matokeo. Anasimulia:
Lakini siku moja nilipokuwa nasoma Biblia yangu, Mungu alinionyesha jinsi Paulo alivyotumia ujuzi wake katika huduma.
Bwana aliniambia, “Bado unaweza kunitumikia katika kijiji hiki. Unaweza kushinda vizingiti na changamoto ikiwa utatii na kutumia ujuzi niliokupa.”
“Asante, Bwana. Najua jinsi ya kuendesha biashara. Je, inawezekana kuanzisha biashara hapa na kuendelea kufikia malengo?”
Kwa mtaji mdogo, nilifungua duka ambapo nauza paneli za solar na vinywaji. Ninachaji simu na betri, pia nina saluni ya kunyoa. Baada ya miezi michache, nilipata marafiki wengi.
Wanakijiji waliacha kutuona kama maadui. Hakukuwa na umeme, lakini waliweza kuchaji simu zao au kununua mfumo mdogo wa sola kutoka dukani kwangu. Viongozi wa msikiti waliniambia wanataka kununua mfumo wa sola na walitaka niwafungie. Hivyo nikafanya hivyo, na nikaweka mistari ya Maandiko katika kila taa niliyoweka.
Kuendesha biashara kuliondoa vikwazo vingi tulivyokuwa tunakumbana navyo, na kulisaidia kujenga daraja imara la kuwafikia makabila katika eneo letu.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza hapa https://afrigo.org/…/missionary-profile-rev-edwin-b-fussi/