Skip to content

“Tuliona mamia ya watu wakimwamini Yesu” – nyakati za wamishenari

Tariku Gebre, Mkurugenzi wa Africa wa Shirika la Horn of Africa Mission
Sehemu ya Pili ya Sehemu ya Pili
Baada ya kuhitimu chuo mwaka 1993, niliwekwa wakifu kuwa mwinjilisti na Kanisa la Bahir Dar Meserete Kristos. Katika siku za mwanzo, niliongoza huduma za injili sehemu mbalimbali—kwenye magereza, kwa watoto wa mitaani, makahaba, vijana wa vyuo vikuu na hata maafisa wa serikali. Tulishuhudia mamia ya watu wakimwamini Yesu, na makanisa mengi yakianzishwa na kuongezeka.
Katika miaka mitano iliyopita nikiwa Mkurugenzi Mkuu wa Horn of Africa Evangelical Mission Engagers (HO-ME), nimeona viongozi zaidi ya 40,000 wakifundishwa na kuwezeshwa, ambao wamechangia kuongeza wanafunzi wapya zaidi ya 130,000 katika mwili wa Kristo. Pia, karibu makanisa 10,000 yameanzishwa na kuongezeka hadi kizazi cha 9 miongoni mwa makundi 32 ambayo hayajafikiwa vya kutosha nchini Ethiopia na katika eneo lote la bara ya Afrika lililobakia.
Hivi karibuni, nimechaguliwa kuhudumu kama Mkurugenzi wa Afrika katika shirika la Horn of Africa (USA). Shauku yangu na tamanio la moyo wangu ni kuongeza uwezo wa kanisa la Afrika katika kupeleka wamishenari, ili kumaliza kazi ya kufikia makundi ambayo bado hayajafikiwa. Tunatamani kuuona mabadiliko barani Afrika, kwa kuwepo kwa vituo vya kupeleka wamishenari kila pembe ya bara.
Ndoto yangu ni kuona mmoja kati ya kila waamini 10,000 wa kiinjili anakuwa mmishenari — kwa utukufu wa Jina lake miongoni mwa mataifa yote.
Tariku Gebre, Mkurugenzi wa Afrika, Huduma ya Horn of Africa.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/story…/missionary-profile-tariku-gebre/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us