fbpx Skip to content

“Wanawake waliopigwa na butwaa”- nyakati za wamisionari

Nilipokua mmisionari mpya huko Madagaska, niliwaalika wanawake wawili waje kunitembelea. Walipokuja niliwapa juisi na biskuti baada ya kuketi, walionekana kushangaa sana huku wakitazamana kwa mshangao. Walisita kunywa, na walisubiri mpaka nilipoanza kunywa na kuchukua juisi yao. Ziara yetu ilipoisha, niliwakumbatia walipokua wakitoka nje na walionekana kushtuka sana. Nilishangazwa ikiwa nimefanya jambo baya. Baadaye, nilipotembelea nyumba ya Wamalagasi, nilingoja kwa muda mrefu, nikiwa na kiu, kabla sijaomba kinywaji. Inavyoonekana kwenye utamaduni huo hupewi chochote mpaka uombe.Hawakumbatiani lakini huweza kupeana busu mara tatu kwenye shavu. Sote tukiwa waafrika, nilichukuliwa haswa na hizi tofauti za kiutamaduni na nikajifunza kufanya kama wao.

Mmisionari wa Afrika Kusini

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us