Wakumbuke Unapokuwa Katika Maombi – nyakati za wamishenari

Tulikutana na watu kutoka Rwanda, Sudan Kusini, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao walikuwa wakingojea ujio wetu kanisani tangu asubuhi. Wengi wao walikuwa hasa wanawake na watoto, na walikuwa wamefika kambini kutokana na vita na hali ya kuteteleka katika nchi zao. Wengi wameendelea kukaa kambini kwa miaka mingi, na bado wanangoja hali ya amani na utulivu kurejea katika nchi zao.
Kuna kanisa la Anglikana katika kambi hiyo ya wakimbizi, na Msomaji wa Maandiko, Bw. Nicholas Naturinda, pamoja na Askofu Msaidizi walitufahamisha kuhusu kazi inayofanyika huko. Tulifurahi kusikia kwamba kanisa linafanya kazi nyingi nzuri katika kambi hiyo, ikiwemo mikutano ya injili, ushirika, na shule kubwa ya msingi yenye wanafunzi zaidi ya 1800.
Tulivutiwa kusikia kuhusu programu za ushauri wa kisaikolojia kwa waathirika wa mshtuko/kiwewe (trauma) ambazo kanisa linaendesha kwa ushirikiano na (Chama cha Biblia cha Uganda) Bible Society of Uganda. Wakimbizi wengi wameathirika kisaikolojia kutokana na ukatili wa kingono, kupoteza wapendwa wao na kupoteza mali, pamoja na maumivu ya kuwa mbali na nchi zao.
Wakumbuke unapoomba.
– Natukunda Agnes Joy, Uganda
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/…/missionary-profile-agnes-joy…/
Soma hadithi zaidi za misheni kupitia https://afrigo.org/shuhuda-za-wamisionari/