Tuliomba kwa ajili ya uponyaji na nikaponywa! – nyakati za wamishenari

Nilikaribishwa na wamishenari wa AIM wa Kanisa la Africa Inland Church kufanya kazi katika Taasisi ya Biblia na Huduma hapa Tanzania (Institute of Bible and Ministry) katika nafasi ya uangalizi (caretaker) mwaka wa 2016, ingawa nilikuwa napafahamu mahali hapo kabla. Fursa ya kufanya kazi mahali hapa ni kudhihirika kwa neema ya Mungu, na siwezi kujisifu kuhusu hilo! Namshukuru Mungu kuwa sasa mimi ni sehemu ya kazi yake hapa Sanga Sanga.
Pia ninaongoza kanisa lililoko Kiloka (takribani maili 30 kutoka Morogoro). Eneo hili lina Waislamu wengi. Watu wanaponiuliza kwa nini ninajisumbua na upandaji kanisa, ninacho waeleza tu ni kwamba ni mpango wa Mungu. Yesu, katika Mathayo 28:19, aliwaambia wanafunzi wake waende kuhubiri injili, kwa hiyo ilinibidi kufanya hivyo! Pia tumeamriwa kuwa nuru katikati ya giza.
– Francis Manungu
Soma zaidi hadithi hii (kwa Kingereza) kwenye https://eu.aimint.org/why-bother-church-planting/