Skip to content

“Tulicheka sana” – nyakati za wamishenari

Mimi na timu yangu tunafanya kazi miongoni mwa watu wanaozungumza Kifaransa na Kiarabu. Kifaransa ni lugha ya kibiashara wakati Kiarabu ni lugha mama kwa majirani zetu wengi. Tangu tulipowasili katika mji huu, mimi na timu yangu tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii kufikisha injili kwa kutumia njia zinazofaa kitamaduni. Kwa hiyo tuliamua kujifunza Hadithi ya Manabii – Taarikh al-anbiya – inayoanza na maisha ya Adam na Hawa na inaishia na Bwana wetu Yesu na jinsi alivyoutoa uhai wake kulipa gharama ya dhambi iliyoingia duniani kupitia Adam na Hawa. Mwisho mwa hadithi hii, kuna wito binafsi wa kukubali zawadi ya wokovu kupitia dhabihu ya Yesu. Maneno ya Kiarabu yaliyotumika huko ni “nakhkhbaloha” yenye maana ya “kukubali”.
Siku moja, niliwasimulia hadithi hii moja ya marafiki zangu wa karibu, na mwisho wa hadithi nilisahau jinsi ya kusema sehemu ya kwanza ya neno kwa hivyo badala yake kwa haraka nikalisema kwa Kifaransa na kusema ” accepte-loha”. Tulicheka sana namna ambavyo ujuzi wangu wa kuchanganya Kifaransa na Kiarabu na tulijikuta tunachanganya maneno mengine pia.
Tangu siku hiyo, mimi na B tumekuwa tukijifunza Biblia pamoja mara 3 hadi 4 kwa juma tukiangalia maisha ya Yesu, unabii juu yake kwenye Agano la Kale, Zaburi na Mithali. Huwa tunasoma naye hadithi za manabii na wakati mwingine kila tunapofika mwisho tunasema pamoja… ” accepte-loha ” na kisha tunacheka kwa sauti kubwa huku tukipeana TANO!
B yuko radhi sana kusoma, kutazama na kusikiliza nyaraka za Biblia pamoja nami. Hata hivyo, yeye hajioni kama chochote isipokuwa M*sl*m. Bado haamini baadhi ya ukweli kuhusu Yesu, ingawa anafurahia kunisaidia kwenye lugha ya Kiarabu. Ombea kwamba neno la Bwana lichome moyoni mwake wakati anapoendelea kulisikia na kulisoma. Omba kwamba macho yake yafunguke na aone kwamba maneno ya Bwana yana uzima zaidi kuliko maneno ya kitabu chake cha kidini! Omba kwamba B siku moja aweze “accepte-loha” zawadi njema ya wokovu kwa ajili yake mwenyewe.
Habiba kutoka Lesotho, akihudumu kaskazini mwa Afrika
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us