Skip to content

“Sikujua niende wapi” – nyakati za wamishenari

Nilikuwa nimeamua moyoni mwangu kwamba baada ya kuhitimu chuo ningekuwa kwenye kazi ya umishenari kwa muda fulani. Sikujua ni kwa namna gani wala ni wapi, hadi siku niliyokutana na rafiki yangu kutoka Msumbiji.
Nilipokuwa shuleni, nilijihusisha na vikundi vya uinjilisti vyuoni, jambo lililonihamasisha kujihusisha na kazi za umishenari. Baada ya kumaliza masomo yangu ya uzamili, niliungana na Life Changers. Ambayo hii ni huduma/mpango wa kuwafikia vijana unaoundwa na wahitimu wa vyuo na walioko vyuo vikuu ambao hujitolea kuwafikia na kuwahudumia wanafunzi katika vyuo na vyuo vikuu.
Nikiwa huko, nilipata rafiki kutoka Msumbiji. Alikuwa mchungaji aliyekuja kwaajili ya mafunzo, na tulipoendelea kuzungumza, nilifahamu hali ya huduma kwa vijana na watoto nchini Msumbiji. Nilisikitishwa sana kujua kwamba hakuna huduma zilizopangwa nchini Msumbiji za kuwasaidia watu kufanya kazi ya huduma katika taasisi za elimu, tofauti na ilivyo Kenya.
Nilikwenda Msumbiji kwa mara ya kwanza na nikafanya kazi ya kufikia watu huko Mocímboa da Praia, kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka 2018. Nikiwa huko, niliungana na Operation Mobilization (OM), ambao pia wanajihusisha na kazi za kibinadamu. Kimbunga kilipiga eneo fulani la Msumbiji, na OM walihitaji mratibu wa kukabiliana na maafa, jukumu ambalo nililikubali.
Bado ninafanya kazi na OM, na sasa tuna takribani vikundi vitano vya wana Mafunzo. Mafanikio yangu makubwa zaidi yalikuwa kuweza kuwasiliana na Wamsumbiji kwa lugha yao. Niliamua kuendelea hata kama sikuwa nimekamilisha vizuri Kireno. Changamoto yetu kubwa zaidi ni kupata vifaa vya kufundishia kwa lugha ya Kireno.
Lenny Karanja, mmishenari kutoka Kenya anayehudumu Msumbiji.
Soma hadithi kamili kwa kingereza kwenye https://afrigo.org/…/missionary-profile-lenny-karanja/…
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us