fbpx Skip to content

“Riziki ya Mungu Dukkawa”- nyakati za wamisionari

Nilitumwa kwenye shule ya umisheni miongoni mwa kabila ambalo halijafikiwa kwa safari yangu ya pili ya umisionari, kwa miaka 2. Kwa kukosa wafanyakazi, nilikuwa na mengi katika maelezo yangu ya kazi. Nilikuwa mwalimu wa darasa la msingi (darasa la 1) na mwalimu wa masomo mawili. Wanafunzi wangu walikuwa watoto wazawa ambao walitoka sehemu za kijijini sana; wengine walikuwa hawajawahi kuona magari hapo awali. Njia kuu ya usafiri kwa safari za mbali ilikuwa ngamia, ambapo kila familia yenye hali nzuri ilikuwa nao. Unaweza kufikiria jinsi ilivyokuwa ya kuchosha kuhakikisha kuwa watoto waliweza kuzungumza Kiingereza katika muhula wao wa pili na kuweza kusoma maneno ya herufi 3 hadi 4 kama kigezo cha kuhitimu kwao katika darasa linalofuata. Hili lilikuwa jukumu gumu zaidi.

Nilikuwa na maelezo mengine ya kazi: mhasibu wa shule, dereva wa shule, kocha wa mpira wa miguu wa shule, mzazi wa bweni la wavulana, na kiongozi wa masomo ya Biblia/wa ibada kwa shule za msingi kwa darasa la 6 na la 3. Majukumu haya yalinifanya niwe na shughuli nyingi kuanzia saa 11:00alfajiri hadi saa 6 usiku kila siku na kupelekea kushindwa kujiandalia chakula changu mwenyewe.

Nilikuwa mmisionari mpya, sikuwa hata na mwaka mmoja shambani, kufanya kazi na shirika ambalo halikulipa mishahara wala posho. Niliishi kwa imani kabisa, nikimtumaini Mungu kukidhi mahitaji yangu. Zaidi ya miezi 4, nilipokea Naira ya Nigeria chini ya 8,000 – sawa na dola 6. Nikiwa mhasibu wa shule, nilikuwa nikilipa msaada ambao ulikuja kwa watendaji wakuu; wengine walikuwa wakipokea makumi na mamia ya maelfu lakini kwangu hakuna chochote kilichokuwa kikitoka nje.

Hii ni kwa sababu kanisa la mtaa ambalo nilikuwa nalo kabla ya kujiunga na umisheni halikuamini katika umisheni wa mwingiliano wa kiutamaduni na hawakuwa tayari kutoa msaada, ingawa baadaye walielewa na kubadilika.

Hata hivyo, Bwana alinitegemeza kupitia jiko la wanafunzi. Niliruhusiwa na mkuu wa shule kula kutoka kwenye chakula cha watoto kwa ajili ya kifungua kinywa, chakula cha mchana, na chakula cha jioni. Hili ilileta unyenyekevu kwa sababu wafanyakazi wengine hawakulazimika kufanya hivyo, lakini BWANA alinifunulia kwamba alitaka nile kutoka kwenye chanzo hicho hadi atakaporudi kwangu. Ilikuwa uzoefu wa kweli kwangu kwa sababu chakula hakikuwa sawa na nilivyozoea, nikiwa mtu wa mashariki kutoka Igbo ambapo ni wapishi wazuri na wanaojali sana ubora wa chakula chetu. Mahali hapa, kwa upande mwingine, palikuwa sehemu ya kaskazini mwa Nigeria yenye ubora tofauti wa chakula. Lakini BWANA aliitumia kunitegemeza huko kwa miaka 2.

Baada ya miaka 2, aliniongoza pamoja na timu nyingine kuanzisha uwanja mpya wa umisheni katika makao makuu ya Kiislamu ya Ukhalifa wa Sokoto wa Nigeria. Katika mpaka huu mpya, kila kitu kilibadilika. Niliolewa, kisha nikawa na watendakazi na marafiki ambao walianza kutuma pesa mara kwa mara ili kutegemeza kile tulichokua tukifanya na sisi tukiwa wamisionari. Lakini huko Dukkawa katika jimbo la Niger, hayakuwa mafunzo madogo ya imani kwangu.

– Ndugu Ugochukwu G.U. ni mmisionari aliye na CAPRO akiwafikia Waislamu wahamiaji wa kaskazini walioko ughaibuni Mashariki mwa Nigeria

share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us