“Nimekuwa mkimbizi kwa miaka minane” – nyakati za wamishenari
Jina langu ni Solomon Babaker kutoka kabila la JumJum. Nimekuwa mkimbizi huko Doro Mabaan, Sudan Kusini, kwa miaka minane. Nilikuwa Muislamu kabla ya 2014, na familia yangu ilikuwa iki amini uchawi na kutembelea waganga. Walikuwa wakinywa marisa (pombe ya kienyeji). Mmishenari Mwethiopia aitwaye Getachew alikuja kwetu; alikuwa akifundisha kundi la vijana kanisani na alikuwa ametoa kazi kwa kikundi cha vijana.
Kazi ilikuwa kushirikisha Habari Njema angalau kwa watu wawili kila juma. Kijana anayeitwa Joseph Idris alikuja kwangu na kushiriki Habari Njema pamoja nami. Jumamosi moja, alinipeleka kwenye kundi kanisani, nami nikampokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wangu. Kisha nikaanza mafunzo ya Biblia pamoja na kikundi hicho. Nilikuwa nikijifunza kuhusu Yesu Kristo katika kundi hilo, na hapo ndipo nilipokutana na Getachew, aliyekuwa akiongoza kundi hilo. Mke wangu pia akawa Mkristo, nasi tunasali pamoja.
Nilipata nguvu katika imani yangu ya Kikristo na katika kushuhudia injili. Kisha, kanisa la Jumjum lilinifanya kuwa mwinjilisti. Wakati huu, nilianzisha kikundi na majirani zangu (wanaume, wanawake, na watoto) ambapo nilishuhudia kuhusu Yesu Kristo. Baada ya muda, nilirudi Wadaga, nchi yangu, na kushuhudia Habari Njema na kabila langu.
Nimekuwa nikifanya hivi angalau mara moja kwa mwaka. Mnamo 2018, nilipata nafasi ya kuhudhuria masomo maalum ya Biblia, kusoma mafunzo huko Juba kwa miezi sita kupitia misheni ya Nubian.