Skip to content

“Nimechoka” – nyakati za wamishenari

Ripoti kutoka kwenye eneo la umisheni huko Sudan Kusini:
Tuna hadithi ya mwanamke kutoka kijiji jirani. Wiki moja iliyopita *Miriam alikuja nyumbani kwetu. Alipofika alijitafutia kiti mwenyewe na kuketi nje ya nyumba yetu. Na hii sio kawaida katika utamaduni wao. Mimi na mke wangu tulitoka na kwenda kumsalimia. Baada tu ya salamu, alisema “Nimechoshwa na maisha ya dhambi ambayo nimekuwa nikiyaishi, nahitaji msaada wenu.”
Tulimwambia kwamba hatuna njia ya kumsaidia katika changamoto aliyotuambia na kwamba Kristo pekee ndiye anayeweza kumsaidia ikiwa atayatoa maisha yake kwa Kristo. Kwa haraka, alisema, “Nataka kuyatoa maisha yangu kwa Kristo.” Tulimsaidia kuelewa kidogo kuhusu wokovu na tukamwombea, na kisha akayatoa maisha yake kwa Kristo. Na baada ya muda si mrefu, alisimama na kuanza kutoa ushuhuda wake hadharani. Tumwombee dada huyu anapoanza maisha mapya katika Kristo.
-Robet & Carol Bett, wamishenari kutoka Kenya
Picha ya mwakilishi kutoka Hadithi za AIM
*sio jina lake halisi
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us