“Nilipewa nyama ya mwana-kondoo aliyekufa”
Mmishenari wa Uganda/Rwanda kwa Wadatoga wa Tanzania: Rosemary AthanasNilizaliwa Tanzania, nikiwa na baba Muganda na mama Mnyarwanda. Nilikulia katika familia ya “Kikristo” ambayo pia haikuona shida kwenda kwa mganga wa jadi mara kwa mara.
Baada ya kumpokea Kristo, nilijiunga na Tanzania Assemblies of God. Nilihudumu kama mwinjilisti mpaka mmishenari mmoja aliponiuliza kama nimewahi kufikiria kuwa mmishenari.
Niliomba kuhusu jambo hilo, na mchungaji wangu aliniandikisha katika kozi ya umishenari katika East Africa School of Missions. Nilipokuwa katika shule ya umishenari, nilikutana na kijana kutoka kabila la Datoga; nikagundua kuwa walikuwa hawajafikiwa na injili.
Miezi sita baada ya mafunzo yangu ya umishenari, niliwasiliana na mmishenari aliyekuwa akiwafikia Wadatoga na nikamwomba aniunganishe niwe miongoni mwao.
Katika siku yangu ya kwanza kwenye huduma ya umishenari, mwenyeji wangu alipika mwana-kondoo mchanga aliyekuwa amekufa kwa siku kadhaa. Kila mtu alisubiri kuona kama ningekula. Nilikula. Huo ulikuwa mtihani, na walifurahi kunikaribisha katika jamii yao.
Bado ninaendelea kueneza injili hapa.
Soma simulizi kamili kwa kiingereza hapa: https://afrigo.org/…/missionary-profile-rosemary-athanas/