Skip to content

“Nilikuwa nimepotea” – nyakati za wamishenari

“Sehemu ya kwanza kati ya tatu”
Nilizaliwa Angola. Niliona mambo mengi mabaya wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kutokana na vita hivyo, sikuwahi kumjua baba yangu.
Mwaka 1993, mimi pamoja na kaka yangu tulilazimika kupelekwa katika kituo cha watoto yatima kilichokuwa na zaidi ya watoto 100, vijana, na watu wazima – kila mmoja akiishi kama vile alivyoona inafaa. Miaka michache baadaye, niliingia kanisani na nikasikia ujumbe wa Injili. Nilijitokeza mbele, wakaomba kwa ajili yangu.
Nilianza kufunzwa na Ndugu Alberto Lucamba Alberto na nikaanza kuhudhuria mara kwa mara kwenye kanisa la UIEA huko Lubango. Mapema sana katika kanisa hilo, nilisikia mahubiri kuhusu umisheni mara kwa mara, na yalinishangaza na kunivutia. Sikuwa na ufahamu wa kujua kwamba ni Mungu alikuwa anaongea. Nilikuwa nasoma masomo ya kemia chuo kikuu. Nilikuwa nafanya vizuri sana, lakini kila nilipoenda chuoni, nilijihisi mwenye huzuni na asiyetii.
Wakati huo huo, mmishenari mmoja aitwaye Dkt. Steve Duncan na Mchungaji Bernardo Chinoia walianzisha kikundi kidogo kanisani kuhusu mambo ya umisheni, kikundi kilichoitwa “Waliotumwa”. Tulizungumza kuhusu umisheni, kile kila mshiriki alikuwa akimfanyia Mungu katika wiki hiyo, na mara nyingine tulifanya safari fupi za kimisheni katika maeneo ya vijijini ndani ya Mkoa wa Huila.
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/…/missionary-profile-frederico…/…
Soma hadithi zaidi za kimishenari kupitia https://afrigo.org/shuhuda-za-wamisionari/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us