“Nilikuwa nikiihubiria miti” – nyakati za wamishenari
Mmishenari na Mhamasishaji nchini Malawi: Felix KalanziNilipoteza wazazi wangu ndani ya kipindi cha miaka mitatu kabla sijafikisha umri wa miaka tisa! Binamu yangu alinilea na alikuwa akinichukua kwenda kanisani kwao. Nilipofikisha miaka kumi, nilimpokea Yesu na Mungu akaondoa huzuni yote niliyokuwa nayo kutokana na kupoteza wazazi wangu. Nikaamua kuwa mhubiri.
Kama mtoto wa miaka kumi aliyezaliwa mara ya pili, mwenye shauku kubwa, nilikuwa nikiihubiria kwa uaminifu na kwa bidii miti iliyokuwa porini nyuma ya nyumba ya binamu yangu, nikiiomba impokee Kristo. Sikupata iliyoongoka hata moja, lakini kanisani nilipata nafasi ya kuandamana na wahubiri wa injili katika kuhubiri nyumba kwa nyumba. Jambo hilo liliniletea furaha kubwa.
Nilipoenda shule ya sekondari, nilijiunga na Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Malawi (SCOM). Baada ya kumaliza shule ya sekondari, nilienda Lilongwe kutafuta kazi. Moto wa kuwa mhubiri ulikuwa unaendelea kuwaka ndani yangu, na nilikuwa nikihubiri kila mahali—kwa wenzangu kazini, magerezani na hospitalini. Nilihisi uharaka wa kumhubiri Yesu kwa wale waliopotea.
Baadaye nilienda katika shule ya umishenari na nikashangaa kujua kuwa mamilioni ya watu wanakufa bila kumjua Kristo. Niliamua kujiunga na kazi ya uhamasishaji nchini Malawi. Pia nimekuwa nikifikia taifa ambalo halijafikiwa ndani ya Malawi huku nikijifunza kutoka kwa wamishenari waliopo hapa jinsi bora ya kuwafikia.
Soma simulizi kamili hapa: https://afrigo.org/stor…/missionary-profile-felix-kalanzi/