Skip to content

“Nilihisi msisimko” – nyakati za wamishenari

Sehemu ya 2 kati ya 3
Mnamo mwaka 1998, nilihudhuria kambi ya vijana iliyoandaliwa na Youth for Christ. Mhubiri alizungumza kila siku kuhusu ni nani anaweza kumtumikia Mungu kupitia umisheni. Nilihisi msisimko na moyo wangu ukaguswa vilevile kama ulivyokuwa wakati wa ibada kanisani ambapo mtu alizungumzia kuhusu umisheni. Niliitikia wito wake wiki hiyo yote. Niliondoka kwenye kambi nikiwa nimeamua kuacha masomo yangu chuoni, kuacha kazi yangu (nilikuwa mhadhiri), na kujiunga na ISTEL, Shule ya Theolojia.
Katika mwaka huo huo, 1998, nilialikwa kushiriki katika safari ya kimisheni kwenye mlima uitwao “O Munda Yo Vaimbo” ambao unamaanisha Mlima wa Theluji. Huko, Mungu alithibitisha yote niliyokuwa nikihisi hapo awali.
Lengo lilikuwa kukaa kwa saa moja tu kwenye mlima huo, kusikiliza ushuhuda wa Mmishenari Inacio Fio, aliyekuwa akiishi hapo, na kujifunza kutokana na uzoefu wake. Baada ya hapo, tulitakiwa kurudi Lubango. Kulikuwa na vijana wanane kutoka kikundi cha “The Sent”, na tulienda pamoja kwa ndege ya MAF (Mission Aviation Fellowship) na Mmishenari Daktari Duncan.
Hivyo basi, niliamua kubaki hapo kwa wiki moja, nikiwa na nguo zile tu nilizovaa, lakini nilikuwa na furaha sana. Kila jioni, kila mfanyakazi kutoka shirika la afya la Kibrazili alisimulia jinsi Mungu alivyo mwita kwenye huduma. Hadithi zao zilikuwa kama visu moyoni mwangu. Kila jioni nilihisi msisimko ule ule… Nikaomba, “Mungu, hii ni nini?”
Soma hadithi yote kwa Kiingereza kupitia https://afrigo.org/…/missionary-profile-frederico…/…
Soma hadithi zaidi za misheni kupitia https://afrigo.org/shuhuda-za-wamisionari/
share
share
Instagram
contact us
contact us
contact us